Home Habari za michezo ZILE TETESI ZA ‘BEKI KISIKI’ NATHAN IDUMBA KUTAKIWA SIMBA ZIMEMUIBUA WAKALA WAKE…KAANIKA...

ZILE TETESI ZA ‘BEKI KISIKI’ NATHAN IDUMBA KUTAKIWA SIMBA ZIMEMUIBUA WAKALA WAKE…KAANIKA UKWELI HUU ..

[the_ad id="25893"]


Wakala wa Beki kutoka DR Congo na klabu ya Cape Town City FC ya Afrika Kusini Nathan Idumba Fasika amekanusha taarifa za mchezaji huyo kuwa mbioni kusajiliwa na moja ya klabu za Tanzania msimu ujao wa 2022/23.

Fasika mara kadhaa ametajwa kuhusihwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, licha ya Uongozi wa klabu hiyo kutosema chochote kuhusu taarifa hizo ambazo zimekua zikisambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii.

Wakala wa Beki huyo Faustin Mukandila amesema, hana mpango wowote wa kufanikisha suala la Fasika kucheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu ujao, na badala yake ana mipango mingine tofauti.

Amesema lengo kubwa la Fasika kwa sasa ni kucheza Ligi kubwa zaidi ya Afrika Kusini, hivyo hakuna la ziada zaidi ya kwenda Barani Ulaya ambapo kuna Ligi za madaraja ya juu zaidi.

“Hakuna Uwezekano wowote kwa mchezaji wangu Nathan Fasika kuja kucheza Tanzania, tunamipango mingi na ofa nyingi za kwenda kucheza nje ya Afrika” amesema Faustin Mukandila

Fasika mwenye umri wa 23 alisajiliwa Cape Town City FC mwaka 2021 akitokea FC Lupopo ya nchini kwao DR Congo.

SOMA NA HII  AZAM FC WAIFUATA NAMUNGO KIBABE...ZAKA ZAKAZI AIBUKA NA HILI JIPYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here