Habari za michezo

KIBU DENIS AKINGIWA KIFUA MSIMBAZI…KASONGO AWAPA ZA USO MABOSI SIMBA KUHUSU USAJILI MPYA…

admin June 10, 2022 2:51 am


BEKI wa zamani wa Simba, Kasongo Athumani  anaamini endapo straika wa timu hiyo, Kibu Denis akivumiliwa msimu ujao atafanya makubwa.

Amezungumza jana Alhamisi ya Juni 9, 2022  kwa njia ya simu, kwamba Kibu ni straika mzuri,  ila ameingia Simba akiwa na changamoto nyingi zilizochangia asianze kwa kishindo.

“Simba wakati inamsajili Kibu kutoka Mbeya City, kulikuwa na mambo mengi, sasa mchezaji ili afanye vizuri anategemea utulivu, soka linahitaji kutumia maarifa mengi, kuliko nguvu bila akili,” amesema na kuongeza;

“Ndio maana Kibu ameanza kuonyesha makali yake mechi za mwishoni, maana yake akili yake imeanza kutulia, binafsi naona ana vitu vingi mguuni kwake.

Amesema wakati Simba inakwenda kufanya marekebisho baadhi ya nafasi, anaishauri kamati ya usajili itulize akili kufanya maamuzi sahihi.

“Ndio maana nimesema mchezaji kama Kibu wanapaswa kumpa nafasi, maana huwezi kupangua timu nzima,” amesema.

PAMOJA NA YOTE YALIYOTOKEA….SIMBA WAPANGUA HOJA YA CHAMA KUVUNJA MKARABA…KUTUA DAR LEO… BAADA YA KUONA MCHEZAJI WAKE AKIZIDI KUWA STAA MKUBWA…MINZIRO AFUNGUKA HAYA KUHUSU GEORGE MPOLE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply