IMEELEZWA kuwa miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye hesabu za kuweza kusajiliwa ndani ya Simba ni pamoja na kiungo Luis Miquissone.
Nyota huyo alikuwa ndani ya Simba msimu wa 2020/21 na alijiunga na Al Ahly msimu wa 2021/22 ambapo kwa sasa bado yupo huku nchini Misri.
Waarabu hao wa Misri msimu huu wamekwama kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuweza kutinga hatua ya fainali.
Luis alikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na hata mikoba ilipokuwa mikononi mwa Didier Gomes bado alikuwa ni chaguo la kwanza.
Anakumbukwa kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat trick ya asisti ilikuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Habari zinaeleza kuwa kwa sasa Simba inafanya mchakato wa kufanya usajili mpya wa kikosi kipya baada ya kupoteza matumaini ya kutwaa taji la ligi ambalo linaelekea kwenda Yanga wenye pointi 64 kibindoni huku Simba wakiwa na pointi 51.