Habari za michezo

BAADA YA KUSHINDWA KUWASAJILI AZIZ KI NA ADEBAYOR…AHMED ALLY AIBUKA NA HILI…ADAI HAWAKUWA NA HADHI…

admin June 14, 2022 7:31 am


Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmedy Ally, amesema Rais wa heshima wa klabu hiyo Mo Dewj, ametenga fedha za kusajili kila mchezaji atakayehitajika katika klabu hiyo.

Ahmedy amesema juzi Juni 11, wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Simba Kisukuru lililopo Tabata, jijini Dar Es Salaamu.

“Kila ambae atasajiliwa atawekwa hadharani wana Simba mtaonyeshwa, wana Simba mtaambiwa.

“Niwaambie tu kwamba safari hii litakufa jitu, tunafanya usajili wa maana sana kwasababu fedha ipo.

“Rais wa heshima, Mohammed dewj ametenga fedha ya kutosha ya kuweza kusajili kila mchezaji ambae tunamhitaji, na hatimae anatua Simba Sc.

“Ukiona tumeacha kumsajili mchezaji pamoja na kwamba ni mzuri lakini jua kwamba fedha walioitaka haifanani na thamani ya ya huyo mchezaji.

Kauli hiyo ya Ahmed Ally ni sawa na kurusha dongo Yanga, ambapo wamemsajili Aziz Ki ambaye Simba wameshindwana  naye kwenye mapatano ya ada ya usajili pamoja na maslahi binafsi, huku Yanga wao wakitoa dau mara mbili ya walilotaka kutoa Simba.

KUHUSU KOCHA MPYA MSIMBAZI…MABOSI SIMBA WAJIFUNGIA NDANI KUCHAMBUA MAJINA YA MAKOCHA WATATU… KUHUSU KUKIPIGA MSIMBAZI MSIMU UJAO…SAIDO NTIBAZONKIZA AFUNGUKA A-Z WALICHOAFIKIANA NA MABOSI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply