Home Azam FC DAH…IDDI NADO NDIO BASI TENA AZAM FC….DAKTARI ADAI OPERESHENI YAKE ILIKUWA KUBWA…

DAH…IDDI NADO NDIO BASI TENA AZAM FC….DAKTARI ADAI OPERESHENI YAKE ILIKUWA KUBWA…


Japo afya yake inazidi kuimarika na kuanza mdogomdogo akipiga mazoezi ya kujiweka fiti, lakini ukweli ni kwamba winga wa Azam FC, Idd Seleman ‘Nado’ atazikosa mechi zilizosalia za kufungia msimu kwa timu hiyo, kwani anatarajiwa kuonekana tena uwanjani Septemba ikiwa ni msimu ujao.

Nado yupo nje ya uwanja kutokana na kuumia goti la mguu wa kulia na hali yake inaelezwa inaendelea kuimarika zaidi kwa sasa, japo kutumika uwanjani ni labda msimu ujao.

Daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa alifunguka jinsi afya ya Nado inavyoendelea vizuri na kwamba programu ya mazoezi ya kumuweka fiti goti lake itamalizika Agosti.

“Operesheni yake ilikuwa kubwa (Anterior Cruciate Ligament), ndio maana alitakiwa akae nje miezi tisa na programu hiyo itaisha mwezi wa nane na tayari ligi ya msimu huu itakuwa imeisha na umeanza msimu mpya,” alisema Dk Mwankemwa na kuongeza;

“Hali yake inaleta matumaini makubwa, anafanya mazoezi hadi ya kukimbia, jambo la msingi tunazingatia kila hatua anayotakiwa afanye ili kupona kabisa, ndio maana atatakiwa kuonekana uwanjani hadi Septemba.”

Nado aliumia akiwa kwenye kiwango kikubwa timu yake ikiichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 Novemba 30, 2021, Uwanja wa Azam Compolex.

Kocha wa timu za vijana za Azam FC, Mohamed Badru alisema anaamini atakaporejea Nado ataongeza chachu ya ushindani kutokana na kipaji alichonacho.

“Ni mchezaji mzuri, anajua kufunga kikubwa ni kumuombea kheri aweze kurejea salama kuendelea na majukumu yake,” alisema.

SOMA NA HII  KUHUSU UFADHILI WA GSM YANGA...ENG HERSI AFUNGUKA MAZITO....ATAJA FEDHA ZINAZOINGIA...