MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema Klabu hiyo itafanya usajili wa wachezaji wanne au watano tu wa kimataifa kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi cha sasa cha Timu hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Juni 15, 2022 dhidi ya Coastal Union amesema tayari Uongozi wa Klabu hiyo unafanya mazungumzo na baadhi ya nyota kadhaa wanaocheza soka katika Ligi ya Afrika Magharibi, Ligi ya Afrika Kusini, Ligi ya Angola na nyota wa Kimataifa aliyewahi kucheza soka la kulipwa Ligi ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo Manara alitumia lugha ya picha kumtaja Morrisoni, kwani kiuhalisia hakuna Ligi ya Afrika Mashariki , japo inafahamika kuwa Mghana huyo alikuwa akikipiga na Simba ambayo iko Afrika Mashariki.
Manara pia amegusia adhima ya klabu ya Yanga kuhusu wapi wanapendelea kwenda kuchukulia Kombe lao ikitokea wakashinda na kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/2022, ambapo amebainisha kuwa tayari klabu ya Yanga imeanza kufanya mazungumzo na mamlaka husika ikiwemo Bodi ya Ligi ili ikiwezekana timu iende ikakabidhiwe kombelake Jijini Mbeya.
Kwa upande mwingine Manara amegusia suala la siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi Duniani (Albino) ambapo amesema anasikitishwa kuona Tanzania ni moja ya nchi zinzowabagua watu wenye ulemavu wa ngozi.
Ameiomba Serikali pamoja na Taasisi zote za Kidini kulivalia njuga suala hili ikiwemo kuelimisha lakini pia kuwapatia watu mafunzo ya kidini kuhakikisha wanakuwa na hofu ya mungu na kuepuka dhambi ya ubaguzi.
Amesisitiza juu ya suala hili kuwafikia hasa watu wa vijijini ambao kwa wingi wao hawana elimu ya kidini na uelewa juu ya