Habari za Yanga leo
Habari za michezo

“AZIZ KI AMTEKETEZA CHAMA” MCHAMBUZI…AMEFUNGUKA HAYA A-Z

Marce Ben Komba May 4, 2024 11:39 am

Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini, Juma Ayo amesema bila Yanga kumsajili kiungo mshambuliaji, Stephanie Aziz Ki basi mpaka sasa Watanzania wangeamini kiungo bora ni Clatous Chama wa Simba.

Ayo amesema hayo kufuatia staa huyo raia wa Burkina Faso kuonesha kiwango bora ndani ya Yanga tangu ajiunge nao huku msimu huu akiwa kinara wa upachikaji mabao mpaka sasa akiwa amefunga mabao 15 na assis 7 kwenye Ligi Kuu.

“Tunamshukuru Mungu kwa Aziz Ki kuja kucheza Ligi kuu ya NBC, maana bila hivyo tungeendelea kudanganywa sana kuwa Chama ndio Namba 10 Bora kuwahi kutokea Tanzania,” amesema Juma Ayo.

KUMBE HUYU KOCHA NDIYO ALIYEMTOA BACCA…DUUH ALISEMWA VIBAYA YANGA YATUMIA MFUMO WA HISPANIA…AISEE!! KUMBE WALISAINI MKATABA HUU