Home Habari za michezo BAADA YA KUONA HALI HALISI ILIVYO…ERASTO NYONI NAYE ASHUKURU MASHABIKI SIMBA…”TULIANZA NA...

BAADA YA KUONA HALI HALISI ILIVYO…ERASTO NYONI NAYE ASHUKURU MASHABIKI SIMBA…”TULIANZA NA TUNAMALIZA WOTE”…


Beki wa Simba, Erasto Nyoni amewashukuru mashabiki wao kwa namna walivyowapa sapoti licha ya kwamba wameshindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu huu.

Yanga tayari wametangazwa mabingwa wapya wa ligi hiyo huku wakisubiri pia kucheza mechi ya fainali ya ASFC dhidi ya Coastal Union inayotarajiwa kuchezwa Julai 2, mwaka huu jijini Arusha.

Simba msimu huu umekuwa mbaya kwao kutokana na kupoteza makombe yote muhimu la Ngao ya Jamii, Ligi Kuu sambamba na la ASFC.

Nyoni alisema, juhudi ambazo wachezaji uzifanya katika timu mashabiki wanachangia kwa hali kubwa chachu ya mafanikio ya timu yao na msimu huu wameanguka wote. “Mashabiki wetu ni watu muhimu sana na wa kipekee, tulianza pamoja tunamaliza pamoja ni jambo la kujivunia sana, kupoteza makombe kila mwanasimba kaumia lakini ndio mpira,” alisema Nyoni.

Alisema wanajitahidi michezo iliyobaki wapate matokeo mazuri licha ya kushindwa kuchukua taji hilo mara tano mfululizo.

Simba imebakiza kucheza na , Prisons (Sokoine) na Mbeya Kwanza (Majimaji).

SOMA NA HII  KUHUSU UWANJA WA SIMBA...MAMBO YAANZA HUKOOO...BARBARA ATINGA 'SITE' NA WATAALAMU...KUANZA NA MAJUKWAA...