Geita Gold FC

TAARIFA RASMI: FIFA WASHUSHA RUNGU LA ADHABU KWA GEITA GOLD…ISHU YA NDAIRAGIJE YAWAPONZA…

admin June 24, 2022 5:10 pm


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeifungia Geita Gold FC kusajili wachezaji hadi litakapomlipa aliyekuwa kocha wake Ettiene Ndayiragije.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), leo Juni 24, kocha huyo raia wa Burundi alifungua madai dhidi ya Geita Gold FC akidai fidia ya kuvunjiwa mkataba pamoja na malipo mengine wakati akifundisha timu hiyo mkoani Geita.

Kwa mujibu wa taarifa ya FIFA, iwapo Geita Gold FC itakuwa haijamlipa kocha huyo, suala hilo litawasilishwa katika kamati ya nidhamu ya FIFA kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

Aidha, TFF imesema inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zinaingia na wachezaji pamoja na makocha kwa kuwa ni moja ya vigezo vya kupata leseni ikiwa ni utekelezaji wa kanuni za leseni ya Klabu (Club licensing Regulations)

KUHUSU DILI LAKE LA KUJIUNGA NA PSG…ZIDANE AVUNJA UKIMYA…ATAJA KLABU ANAZOWEZA KUFUNDISHA ULAYA… TANZANIA YAZIDI KUPAA KIMATAIFA…FIFA WAIPANGA NA UFARANSA KOMBE LA DUNIA…RATIBA NZIMA IKO HIVI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply