Uwanja Mpya yanga GSM
Yanga SC

KUHUSU UWANJA MPYA WA YANGA…HAYA HAPA YANAYOMPA SIFA MBADALA GSM…

admin May 15, 2026 6:11 pm

Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amerusha jiwe gizani akisema mfadhili wa klabu hiyo Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ hana tamaa katika uwekezaji wa uwanja wa klabu hiyo.

Kamwe amesema kama GSM angekuwa na tamaa kwenye umiliki wa uwanja huo angeweza kuhitaji asilimia 80 kwake na 20 kwa klabu hiyo.

Kamwe amesema GSM amekuwa hana maneno mengi ambapo sasa baada ya maneno yake ya Yanga bingwa watamuongezea maneno mengine hana tamaa.

“Unajua kuna wakati unaweza kuwa na tamaa lakini GSM ni tofauti sana hebu angalia anataka asilimia 50 tu lakini ingekuwa mwingine angehitaji hata asilimia 80 ziwe kwake na klabu tubaki na 20,”amesema Kamwe huku akishangiliwa na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

“Sisi Yanga tunakushukuru kwa moyo wako unatupa somo kwamba tuache tamaa kwenye maisha yetu na nadhani GSM amekuwa hataki mambo mengi kuna ile kauli yake ya Yanga bingwa lakini sasa tumuongezee maneno haya hana tamaa.

Yanga imesaini makubaliano na kampuni hiyo kwenye ujenzi wa uwanja huo mpya ambao utajengwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo makao makuu ya klabu hiyo ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Yanga Kumiliki Asilimia 50 ya Uwanja wao Mpya.

RAIS wa Yanga injinia Hersi Said amesema mradi wa ujenzi wa uwanja mpya wa klabu hiyo, utawafanya kumiliki asilimia 50 huku mwekezaji akimiliki 50.

Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini ya mradi huo Hersi amesema, kampuni ya GSM imeonyesha kutotaka tamaa katika umiliki wa uwanja huo kwa kutaka asilimia 50 pekee za umiliki.

Hersi amesema maamuzi hayo yamewapa faraja uongozi wa klabu hiyo, akisema hatua hiyo imeupunguzia mzigo klabu kwa kuwa na nguvu katika mradi huo.

“Wakati tunajadiliana juu ya ujenzi wa uwanja nilishangaa sana kwanini Ghalib Said Mohammed (GSM) haukutumia akili yako ya majadiliano ya umiliki wa mradi,”amesema Hersi.

“Wakati tunajadiliana ukasema unataka kumiliki asilimia 50 pekee za mradi huu hatua ambayo itaifanya klabu yetu nayo kumiliki asilimia 50, hii ni hatua kubwa.”

Aidha Hersi ameongeza kuwa Yanga katika mradi huo mchango wake ni mkubwa ni ardhi wakati GSM ikifanikisha jukumu la uwezeshaji wa kifedha katika kufanikisha uwanja huo.

“Hapa Jangwani tuna eneo lenye ukubwa wa skwea mita 35,000, jukumu letu litakuwa kuwezesha eneo la ujenzi na GSM itafanikisha jukumu la kifedha.

NINI KIMEMKUTA NABY CAMARA SIMBA…..HUU HAPA UKWELI USIOSEMWA… ZA NDAAANIII KABISAAA…..MASTAA HAWA 6 ‘HAWANA CHAO’ NDANI YA YANGA LIGI IKIISHA…