BAADA ya kufahamika kuwa mshambuliaji wa Vipers ya Uganda, Cesar Lobi Manzoki raia wa Afrika Kati anaondoka ndani ya kikosi hicho, mabosi wa timu hiyo wamemuwekea ngumu kwa kudai kuwa mshambuliaji huyo bado ana mkataba huku mwenyewe akisema anakuja nchini hivi karibuni.
Manzoki anatajwa kufanya mazungumzo na Simba na Yanga kila moja kwa wakati wake huku mshambuliaji akidaiwa kuwazimia simu mabosi wa Simba na kuelekea DR Congo licha ya kutumiwa tiketi ya kuja nchini.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Vipers, zinasema kuwa mshambuliaji huyo ambaye msimu huu amefanikiwa kuibuka mfungaji bora hawezi kuondoka ndani ya timu hiyo kwa kuwa amesaini mkataba wa miaka minne huku mwenyewe akidai kuwa alisaini miaka miwili tu ambayo imefika ukingoni.
โManzoki ameingia kwenye utata na klabu yake kwa sababu klabu inadai kwamba alisaini mkataba wa miaka minne mwaka 2020 wakati anajiunga nayo kutokea AS Vita, mkataba uligharimu kiasi cha Dola 150,000 (Sh mil 348.6) na mshahara wa Dola 15000 (Sh mil 34.8).
โLakini mwenye anachosema wakati anajiunga nayo alisaini mkataba wa miaka miwili ambayo mwisho wake mwezi huu na hii imejitokeza baada ya kuwepo kwa ofa za kutoka Simba na Yanga maana kwa sasa mchezaji amerejea DR Congo ila kwa sasa Vipers wameomba nakala ya mkataba wake kwenye Shirikisho la Soka Uganda (FUFA),โ alisema mtoa taarifa.
Alipotafutwa mshambuliaji huyo kutokea DR Congo ambapo alivyouliza alijibu kwa kifupi kuwa anajiandaa kuja Tanzania bila ya kutaja itakuwa kwenye timu gani.