Habari za Yanga
Habari za michezo

INJIANIA HERSI AFUNGUKA YAJAYO ATAJA KUKOSA NGAO YA JAMII

Staff Desk September 3, 2023 6:45 pm

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said, ameweka wazi kuwa, kukosa taji la Ngao ya Jamii sio mwisho wa mapambano, hivyo nguvu kubwa inawekezwa kwenye mashindano yaliyopo mbele yao ili kupata matokeo mazuri.

Yanga ilikuwa inatetea taji la Ngao ya Jamii baada ya kulitwaa msimu wa 2022/23, kwenye fainali dhidi ya Simba msimu huu ilipoteza taji hilo kwa kufungwa penalti 3-1.

Injinia Hersi amesema nguvu kubwa kwa kilichotokea ni sehemu ya mpira, hivyo wanapambana kufanya vizuri kwenye mashindano mengine ambayo wanashiriki ili kutwaa mataji.

Mashabiki wa Yanga wanapaswa watambue kwamba bado kuna safari ndefu, tulikuwa tunahitaji kutwaa Ngao ya Jamii lakini tumeikosa, sasa nguvu kubwa ni kutetea mataji mengine tuliyotwaa ikiwa ni Ligi na Azam Sports Federation.

“Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, huku pia tunahitaji kuona timu inafika mbali, tunaamini hilo linawezekana, tuzidi kushirikiana kwa ajili ya kuona haya yote yanatokea,” alisema Injinia Hersi.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga itacheza dhidi ya Al Merrikh ya Sudan kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi.

MKUDE AIBUA ‘ZONGO’ TIMU YA TAIFA….KOCHA TAIFA STARS AULIZWA MASWALI MAGUMU… JANJA JANJA YA MORRISON KWISHA….APIGWA PINI NA WANAJESHI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply