Home Habari za michezo A-Z JINSI MASHABIKI WALIVYOMUAGA WAWA JANA…AMIMINIWA MAPESA KILA KONA YA UWANJA…NDEMLA AFANYA...

A-Z JINSI MASHABIKI WALIVYOMUAGA WAWA JANA…AMIMINIWA MAPESA KILA KONA YA UWANJA…NDEMLA AFANYA KITUKO…


Dakika 90 zimekamilika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zikiwaacha Mtibwa katika maumivu makali ya kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa Simba Sports Club.

Magoli ya Simba katika mchezo wa leo yalifungwa na Pape Sakho na goli la kujifunga la Shaaban Kado alieshindwa kudhibiti mpira uliopigwa na Peter Banda.

Kiungo wa Mtibwa Hamis Ndemla alioneshwa kadi nyekundu hivyo Mtibwa wakamaliza mchezo wakiwa pungufu.

Mbali na ushindi huo wa Simba, vile vile mechi ya leo ilikuwa inatumika kumuaga beki wao anaemaliza Mkataba Pascal Wawa, ambae baada ya mchezo alikwenda jukwaani kuwaaga mashabiki ambao kwa upendo walikua wakimtunza fedha huku wengi wakiwa na Picha na mabango ya mchezaji huyo.

SOMA NA HII  KISA 'VIBE' LA KIBINGWA LA SIMBA DAY....M-BET TANZANIA WAIBUKA NA KAULI YA KIBABE KUHUSU UDHAMINI WAO...