Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MAYELE ANASIFIWA SANA KILA KONA…MPOLE AVUNJA UKIMYA…AWACHANA WANASIFIA WAGENI…

BAADA YA KUONA MAYELE ANASIFIWA SANA KILA KONA…MPOLE AVUNJA UKIMYA…AWACHANA WANASIFIA WAGENI…


Straika wa Geita Gold, George Mpole amewataka Watanzania kuthamini wachezaji wazawa tofauti na wanavyowachukulia.

Akizungumza jana, Mpole alisema licha ya wao kutozungumzwa sana ila wanafanya kazi kubwa ingawa hawapewi sifa kama ambavyo wageni wamekuwa wakiimbwa kila siku.

“Watanzania wanapaswa kujifunza kuthamini vya kwao sina maana wageni hawafanyi mambo makubwa ila mzani ni lazima ubalansi licha ya ukweli wenyewe tunajifunza kutoka kwao,” alisema na kuongeza;

“Siongei kwangu binafsi ila ni kwa wazawa wote, wapo ambao wanaonyesha uwezo mkubwa kuliko hata hao wageni ila kwa bahati mbaya tunawasahau na kuthamini vya nje jambo tunalopaswa kubadilika.”

Mpole ndiye kinara mzawa mwenye mabao 15 kwenye Ligi Kuu Bara. Nyota wa Yanga, Fiston Mayele anaongoza msimamo wa wafunga akiwa na mabao 16.

SOMA NA HII  MGUNDA : TUNAENDA KUICHAKAZA TIMU YENU YA WANANCHI BILA HURUMA KESHO...