Home Habari za michezo GAMONDI:- SIMBA INA UBORA WAKE…..YANGA HAIJAKAMILIKA…KUNA MAPUNGUFU MENGI…

GAMONDI:- SIMBA INA UBORA WAKE…..YANGA HAIJAKAMILIKA…KUNA MAPUNGUFU MENGI…

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema baada ya kuisoma Simba kwa dakika 180, tayari amepata dawa ya kuimaliza katika mchezo wa Derby utakaopigwa Jumapili hii uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mchezo huo Yanga watakuwa ugenini Jumapili ya Novemba 5, mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 11:00 jioni.

Gamondi alisema amefanikiwa kuwasoma wapinzani wao katika michezo miwili ameona ubora na madhaifu yao na kuyafanyia kazi kabla ya kukutana nao.

“Nimeiona Simba, ina ubora na udhaifu wake, pale kwenye udhaifu ndipo tunapotaka kuutumia ili kupate ushindi kwenye mchezo wetu wa Jumapili,” alisema kocha huyo raia wa Argentina.

Hata hivyo alisema hata timu yake nayo haijakamilika, badala yake ina mapungufu ambayo anayafanyia kazi hasa idara yake ya ushambuliaji na mabeki.

“Nyuma tumekuwa na tatizo ya kuruhusu mabao, lakini pia tumekuwa tukikosa sana mabao hasa washambuliaji, angalia mechi zeti nyingi zinaamuliwa na viungo, sehemu ambayo tuna ubora mkubwa kwa sasa,” alisema kocha huyo.

Gamondi ametabiri kuwa itakuwa ni mechi nzuri na yenye mbinu kali kwa makocha na ufundi mwingi mwingi kwa wachezaji wa pande zote mbili.

“Itakuwa ni mechi nzuri mbinu na ufundi, tunajiandaa kwa ajili ya kutafuta ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri ya mbio zetu za kutwaa ubingwa wa ligi kuu,” alisema Gamondi.

Yanga inashuka dimbani imekusanya pointi 18 baada ya kucheza mechi saba huku Simba pia wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza michezo sita.

Gamondi alitumia dakika 90 za kwanza za mchezo wa robo fainali ya AFL ambapo alitua kwa Mkapa kutazama mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kutoa sare ya mabao 2-2.

Mchezo mwingine ambao Gamondi aliweza kuushuhudia ulikuwa ni ule wa dhidi ya Ihefu wa ligi kuu ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kocha Gamondi atakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa anaipa ushindi yanga mara baada ya msimu uliopita Yanga kupoteza kwa

SOMA NA HII  KWISHA KAZI...WAMOROCCO WAFANYA KUFURU DAU LA KUMNG'OA CHAMA..SIMBA WAKUBALI KIAINA