Home Habari za michezo HII HAPA TIMU ILIYOIONYESHA UBABE WA KIFEDHA SIMBA NA KUMNUNUA BWALYA KWA...

HII HAPA TIMU ILIYOIONYESHA UBABE WA KIFEDHA SIMBA NA KUMNUNUA BWALYA KWA DAU NONO…YANGA WATAJWA…


Mchezo wa Simba na KMC utakuwa maalum kwa ajili ya kumuaga kiungo wao mshambuliaji Larry Bwalya anayetarajiwa kuondoka mara baada ya mchezo huo.

Bwalya moja ya wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa ndani ya timu hiyo akitokea Zambia anakwenda kujaribu maisha yake sehemu nyingine huku habari za ndani ikidaiwa nyota huyo tayari amemalizana na Amazulu ya nchini Afrika Kusini.

Katika taarifa iliyotolewa na Simba, walimtakia mafanikio mema nyota huyo huku wakisita kutaja ni timu gani ambayo atakwenda kukipiga kwa madai ya matakwa ya kimkataba kwa pande zote mbili. β€œTumefikia makubaliano ya kumuuza kiungo mshambuliaji Bwalya kwa timu ambayo hatutaiweka wazi kwa sasa kutokana na matakwa ya kimkataba, atacheza mchezo wetu na KMC na baada ya hapo ataruhusiwa kuondoka kwenda kijiunga na timu yake mpya ambayo inahitaji kuanza maandalizi ya msimu hivi karibuni.”

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 akitokea Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo sasa amesalia na mmoja huku ikidaiwa amesaini miaka miwili na Amazulu hivyo atacheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Bwalya amechangia katika mafanikio ya Simba hivi karibuni huku mashabiki wakipenda zaidi mbwembwe na matumizi yake ya mguu wa kushoto. Awali wakati anatua Tanzania kujiunga na Simba hata Yanga walishafanya nae mazungumzo huku ikijulikana kwamba angeenda Jangwani lakini mambo yakabadilika. Simba imepanga kupukutisha mastaa kadhaa tayari kujipanga upya.

SOMA NA HII  NABI:- HUYU MZIZE HUYU...IPO SIKU NAWAAMBIA