Home Habari za michezo HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOAMUA ‘KUTEMANA KISAIKOLOJIA’ NA RALLY BWALYA…KMC YATAJWA…

HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOAMUA ‘KUTEMANA KISAIKOLOJIA’ NA RALLY BWALYA…KMC YATAJWA…


Uongozi wa Simba umefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wao mshambuliaji Rally Bwalya kwa timu ambayo hawajaiweka wazi kutokana na matakwa ya kimkataba.

Taarifa rasmi iliyowekwa kwenye Simba App, imeeleza kuwa, Bwallya atacheza mchezo wake wa mwisho Jumapili hii dhidi ya KMC na baada ya hapo ataruhusiwa kuondoka kwenda kujiunga na timu yake mpya kuanza maandalizi ya msimu (Pre Season).

taarifa hiyo imeeleza, kwa heshima ya mchezaji ambaye amedumu na Wekundu hao wa Msimbazi kwa misimu miwili, watautumia mchezo huo dhidi ya KMC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar, kumuaga rasmi nyota huyo wa Zambia.

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 kutoka Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo mpaka anaenda na timu mpya alikuwa amebakisha kandarasi ya mwaka mmoja.

Kwa misimu miwili aliyodumu na Simba SC, Bwalya ameisaidia Simba kushinda mataji matatu ikiwemo kushinda mataji ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Kombe la Mapinduzi pamoja na Ngao ya Jamii.

Bwalya ameisaidia Simba kufikia robo fainali ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020-21 na Kombe la Shirikisho kwenye msimu wa 2021-22.

SOMA NA HII  MERIDIANBET YAMULIKA MAISHA YA WATU WASIOONA....!!