Home Habari za michezo KLABU BINGWA ZA DUNIA MPINZANI WA YANGA AIBUKIA NAFASI YA TATU

KLABU BINGWA ZA DUNIA MPINZANI WA YANGA AIBUKIA NAFASI YA TATU

African Football league

Wapinzani wa Yanga kundi D kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri, imemaliza nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa klabu baada ya kuifunga Urawa Red Diamonds kwa mabao 4-2.

Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Prince Abdullah Al-Faisal uliopo Jeddah Saudi Arabia, mabao ya Al Ahly yamefungwa na Yasser Ibrahim 19′, Perce Tau 25′, Yasser Ibrahim akijifunga katika dakika ya 60, na Ali Maaloul akifunga akaunti ya mabao dakika ya 90+.

Mabao mawili ya kufutia machozi ya Urawa Red Diamonds yamefungwa na wachezaji José Kante dakika ya 43 na Alexander Scholz akifunga dakika ya 54.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly inaongoza kundi kwa pointi tano ikicheza mechi tatu huku Yanga ikishika nafasi ya pili na pointi tano baada ya kucheza mechi nne.

Kwenye mchezo wa kwanza Ahly akiwa ugenini alipata sare ya 1-1 dhidi ya Yanga, huku ikitarajiwa kucheza mchezo wa marudiano Machi 1, 2024 na Yanga itakuwa ugenini, Cairo, Misri.

SOMA NA HII  BODI YA LIGI YAILAMU YANGA KWENYE DABI YA KARIAKOO, KISA HIKI HAPA