Home Habari za Simba MAMA SAMIA:- SIMBA NA YANGA WEKENI MAGOLI NYAVUNI…MIL TANO TANO BADO ZIMEJAA

MAMA SAMIA:- SIMBA NA YANGA WEKENI MAGOLI NYAVUNI…MIL TANO TANO BADO ZIMEJAA

Habari za Simba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwapa nguvu vilabu vya Simba na Yanga ambao wapo kwenye michuano ya kimataifa ili wazidi kupambana zaidi na kupata ushindi kwani Tsh milioni 5 anazotoa kwa kila bao wanalofunga bado zipo.

Rais amesema hayo leo akiwa Dar es salaam katika Sherehe za maadhimisho ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).

“Niwapongeze Wanangu wa Yanga na Simba kwa kuitumia vizuri fursa niliyowapa ya goli moja milioni 5 wameitumia vizuri sana, kwa hesabu nilizonazo nadhani Yanga wameshalamba milioni 30 na Simba jana milioni 35 na nyuma nadhani walikula 5 kwahiyo niwapongeze kwa kuitumia vema fursa hii, niwapongeze na ni imani yangu kwamba ile kasi iliyopo miguuni ya milioni 5 kwa goli itaendelea kuwepo huko mbele milioni 5 zitakapoondoka”

“Kwa sasa hivi niwahakikishie wale waliokuwa wakitania jana, niliona utani nampigia Msigwa namwambia ‘ebu maliza mpira haraka mimi pesa zimeisha’, nataka niwahakikishie kwamba Mama bado anazo wekeni mipira kwenye wavu jengeni jina la Nchi yetu, bado zipo,” amesema Rais Samia.

Simba jana alifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 7-0 dhidi ya Horoya na Guinea na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga nae akiwa nyumbani leo atakuwa na kibarua cha kusaka alama tatu mbele ya US Monastir ya Tunisia ili
kujihakikishia anakwenda hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

SOMA NA HII  MAYANGA ATENGENEZEWA UFALME MITBWA SUGAR...KOCHA ATHIBITISHA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here