Home Habari za michezo ISHU YA YANGA NA AZIZ KI SASA NI KAMA KUMSUKUMA MLEVI TU…MWENYEWE...

ISHU YA YANGA NA AZIZ KI SASA NI KAMA KUMSUKUMA MLEVI TU…MWENYEWE AFUNGUKA A-Z MCHAKATO ULIVYO…


Aziz KI amebakiza asilimia 10 tu kumalizika na sasa mwenyewe amefunguka akifichua kwamba kila kitu kitafikia tamati wiki ijayo wakati akatapokutana uso kwa uso na mmoja wa vigogo wa klabu hiyo atakayemfuata kukamilisha palipobakia.

KI amesema hatma ya usajili wake kuja Tanzania kuichezea Yanga imebakiza asilimia 10 pekee na kwamba kama mambo yatakwenda sawa wiki ijayo kila kitu kitamalizika.

Mshambuliaji huyo anayemalizia mkataba wake na ASEC Mimosas ya Ivory Coast alisema; “Kila kitu kinakwenda vizuri kuna uwezekano mkubwa nikaja kucheza Tanzania, kuna mtu nitakutana naye wiki ijayo kama ikiwa hivyo kila kitu kitamalizika.”

Ingawa, KI aligoma kutaja jina la kigogo huyo ila inafahamika kuwa bosi mmoja mzito wa GSM ndiye anayetakiwa kusafiri mapema wiki ijayo kwenda kumaliza dili hilo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia KI kuanza kuwasha moto akiwa na timu yake ya taifa ya Burkinafaso ambapo katika mchezo wa juzi Juni 7 dhidi ya Eswatini ugenini alifunga bao lake la kwanza akiwa na jezi ya timu ya Taifa.

KI aliyeingia kipindi cha pili dakika ya 81 akichukua nafasi ya Gustavo Sangare alifanikia kufunga bao la kiufundi dakika ya 85 wakati taifa lake likiibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Usajili wa KI kuja Yanga inawezekana ukawa ndio usajili wa jina kubwa la timu hiyo kwa msimu ujao ambapo mabosi wa GSM wamekuwa wakikutana na wakati mgumu kufutia kocha wa Yanga Nasreddine Nabi kusisitiza kwamba anamtaka staa huyo kuboresha safu yao ya ushambuliaji.

Tayari mapema Yanga walimtuma mhandisi Hersi Said nchini Morocco wakati KI akiwa na klabu yake ya ASEC ilipokwenda kucheza dhidi ya RS Berkane ambapo walifikia hatua nzuri kisha mshambuliaji huyo kusaini mkataba wa awali na Yanga, licha ya pia kuhusishwa na Simba.

Credit: MwanaSpoti.

SOMA NA HII  UTAMU WA KEKI UKO KWENYE SLOT HII YA PESA NDANI YA MERIDIANBET CASINO...