Home Tetesi za usajili KUELEKEA MSIMU UJAO…TARAJIA KUMUONA KIUNGO HUYU MWINGINE MZAWA AKIKIPIGA MSIMBAZI…ISHU YOTE IKO...

KUELEKEA MSIMU UJAO…TARAJIA KUMUONA KIUNGO HUYU MWINGINE MZAWA AKIKIPIGA MSIMBAZI…ISHU YOTE IKO HIVI…

SIKU chache baada ya kuanza dili na wachezaji wa kigeni 13 kwa nia ya kupata wakali watano, mabosi wa Simba wapo hatua ya mwisho kuinasa saini ya kiraka mzawa anayekipiga Kagera Sugar anayemudu zaidi ya nafasi moja uwanjani.

Kiraka huyo ni Nassor Kapama anayeweza kucheza kama mshambuliaji, kiungo na beki kitu kimewavutia Simba. Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba mabosi wa timu hiyo wamefanya mazungumzo mara mbili na Kapama ambayo kiujumla yamefikia pazuri.

Simba kwa usiri mkubwa walimtumia tiketi ya ndege kutoka Bukoba kuja Dar es Salaam na kuzungumza naye kwa mara ya kwanza.

Inaelezwa baada ya hapo wiki iliyopita wakati Ligi Kuu Bara imesimama, Kapama alikutana tena na mabosi hao akiwa kwenye mapumziko yake na walikubaliana pesa ya usajili, mshahara na mambo mengine ya msingi.

Kigogo mmoja wa Simba, aliyeomba kutotajwa jina alisema mazungumzo ya awamu ya pili yameenda vizuri kiasi kwamba walikubaliana katika masuala yote ya kimaslahi na mengine muhimu kutokana na kuhitaji huduma ya mchezaji huyo msimu ujao.

Katika ligi msimu huu Kapama licha ya kucheza kama beki wa kati, lakini anamudu nafasi ya kiungo inayochezwa kwa sasa pale Msimbazi na Jonas Mkude, Taddeo Lwanga, Sadio Kanoute na wengine, huku akicheza kama mshambuliaji , akiwa na mabao mawili na asisti tatu kwa sasa.

Kabla ya kutua Kagera, Kapama aliwahi kucheza Ndanda, Ruvu Shooting na Coastal Union na mkataba wake kwa Wakata Miwa wa Kagera unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Alipotafutwa Kapama,  alikiri kuzungumza kwa awamu mbili na Simba na kwamba jambo hilo lilikamilika kila kitu kitawekwa wazi na kuonekana timu hiyo msimu ujao.

“Jambo hili likikamilika nadhani kila kitu kitakuwa wazi ila mazungumzo yetu mara zote mbili yamekwenda vizuri na tumekubaliana,” alisema Kapama aliyegoma kuongeza mkataba mpya Kagera licha huu wa sasa kufikia ukingoni mwisho wa msimu. 

Naye Katibu Mkuu wa Kagera, Ally Masoud alisema alizungumza na Kapama na alikubali amefanya mazungumzo na Simba yamefikia pazuri ila hawajui kama kasaini mkataba. “Tumewapa fursa ya kuzungumza na timu nyingine zinazo wahitaji wachezaji wetu ambao mikataba yao inaelekea ukingoni kwani tunaamini wanaongeza tahamani zao,” alisema Masoud na kuongeza;

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTEMWA YANGA ...NYOTA YA KABWILI YAZIDI KUWAKA...AKIMBILIWA NA MBEYA CITY..

“Mwisho wa wiki hii tutakutana na Kapama kuzungumza nae tena kama atakuwa tayari kuongeza mkataba kwetu au dili lake la Simba litakuwa tayari kama ambavyo tunafahamu.”