Home B KISA MISIMAMO YAKE….MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA MWAKINYO…AJIWEKA HATARINI KUFUTWA KWENYE REKODI...

KISA MISIMAMO YAKE….MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA MWAKINYO…AJIWEKA HATARINI KUFUTWA KWENYE REKODI ZA DUNIA..


Mambo yanazidi kumuendea kombo bondia Hassan Mwakinyo baada ya kuporomka kwa mara nyingine kwenye ubora.

Wiki iliyopita bondia huyo namba moja nchini aliporomoka kwa nafasi 16, kutoka ya 17 hadi 33 duniani kwenye uzani wake wa super welter.

Jana ameporomoka tena kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 35, huku wabobezi wa ndondi nchini wakieleza kuwa kutocheza muda mrefu ndiko kunamporomosha bondia huyo kwenye ubora.

Mara ya mwisho Mwakinyo anayeishi Florida Marekani kwa sasa, alipigana Septemba mwaka jana  na kutetea ubingwa wa Afrika (ABU) kwa Technical Knock Out (TKO) dhidi ya Julius Indongo.

Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka huu alivuliwa mkanda huo na ule wa WBF, vyama vyote vikibainisha kuwa amekiuka kanuni zao kwa kutoitetea kwa wakati.

Tangu amewasili Marekani, miezi kadhaa iliyopita Mwakinyo amekuwa akijifua bila kupigana, huku meneja wake nchini, Huzeifa Huzeifa akieleza bado hawajapata bondia wa levo ya Mwakinyo ambaye kabla ya kuporomoka alikuwa ni wa 17 duniani mwenye nyota nne akihitaji moja kufikia rekodi ya mabondia bora wa dunia wenye nyota tano.

Inaelezwa kama hatapigana hadi Septemba mwaka huu, mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec) utamuondoa kwenye renki kulingana na kanuni zake.

“Kutokucheza muda mrefu ndiko kuna mgharimu Mwakinyo, kama nilivyowahi kusema nchi ambayo anaishi kwa sasa kupata bondia wa levo yake, ili akubali kucheza naye kwanza ataangalia pesa au mikanda mikubwa ya WBA, WBC au WBO ambayo yote Mwakinyo hana,” anasema rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC)”. Chaurembo Palasa.

Amesema bondia akikaa mwaka mmoja bila kupanda ulingoni anaonekana hayuko hai ‘inactive’ ingawa akicheza anarudishwa.

Wiki iliyopita menejimenti ya Mwakinyo iligomea pambano dhidi ya Julio de Jesus Rodriguez huko Jamhuri ya Dominicia kutokana na rekodi ya mpinzani wake ambaye ni wa 425 duniani.

SOMA NA HII  MSEMAJI AZAM FC AJIINGIZA KWENYE LIGI YA UBISHANI KUHUSU UWEZO WA MORRISON....ADAI HANA UBORA WOWOTE...