Home Uncategorized ANDRES PALOP KIPA WA ZAMANI WA VALENCIA APONA VIRUSI VYA CORONA

ANDRES PALOP KIPA WA ZAMANI WA VALENCIA APONA VIRUSI VYA CORONA


KIPA wa zamani wa klabu ya Valencia na Sevilla, Andres Palop hatimaye ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kuugua ugonjwa wa COVID19   unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Palop alilazwa hospitali kwa siku 12 akipambana na Virusi vya Corona kwa kuhakikisha anarejea katika afya yake ya kawaida.
 Hispania  ni moja kati ya nchi ambazo zimeathirika kwa kiasi kikubwa na virusi vya corona ingawa kwa sasa Marekani inaongoza ikifuatiwa na Italia kwa kuwa na vifo vingine kutokana na virusi hivyo.
Palop (46) ambaye alikaa hospitali kwa siku 12 kwa sasa afya yake iko vizuri na  ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupimwa tena na kukutwa hana Virusi vya Corona.
 Kipa huyo alisema anawashukuru wote ambao walikuwa wanamsapoti katika kipindi kigumu hasa alipokuwa hospitali.
“Asante  kwa wote ambao walijitolea kwa moyo mmoja kuhakikisha wananisapoti nikiwa mgonjwa hasa wale ambao walikuwa wakiangalia familia yangu wakati mimi na matatizo wapo ambao walikuwa wananitumia meseji na kunipigia simu kujua ninaendelea vipi zaidi ni washukuru wote,” alisema Palop  na kusisitiza kuwa watu wanatakiwa kujilinda na kutulia nyumbani.

SOMA NA HII  UBABE WA YANGA WAIHAMISHA GEITA GOLD