Home Habari za michezo SAKHO NAYE ANYOOSHA MIKONO SIMBA…WAKALA WAKE AGUNGUKA A-Z…AZAM FC WAHUSISHWA..

SAKHO NAYE ANYOOSHA MIKONO SIMBA…WAKALA WAKE AGUNGUKA A-Z…AZAM FC WAHUSISHWA..

Habari za Simba

Wawakilishi wa Mchezaji Pape Ousmane Sakho hawaridhishwi na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa Mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.

Kutokana na hilo kwa mujibu wa taarifa tulizozipata ni kuwa kuna baadhi ya ofa watazifikisha Msimbazi kumhusu Mteja wao ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili Sakho aweze kuondoka kusaka changamoto mpya.

Sakho alisaini kandarasi ya miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi, akiwa ametumikia miaka miwili huku kipengele cha mkataba kikimtaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili avunje mkataba wake, tayari ameshaandika barua.

Wanaamini Kijana anastahili muda wa kucheza zaidi, ijapo mpaka sasa bado hakuna ofa mezani kwa Simba huku zikitarajiwa mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo, inatajwa kuwa huenda kiungo huyo akatimkia Azam FC ambapo inaelezwa kocha mpya wa timu hiyo ambaye pia ni msenegal wanamahusiano toka alipokuwa akicheza kwao.

Uvumi huu unaweza kuwa na nguvu zaidi haswa ambapo Azam kuelekea msimu ujao nao wamejizatiti kufika hatua kubwa kwenye mashindano ya CAF huku wakitazamia pengine kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa endapo wataibuka na ubingwa wa kombe la FA.

SOMA NA HII  WAWA AWAFUNIKA CHAMA NA MIQUISSONE SUDANI