Home Uncategorized SADIO MANE ALICHANGANYA MAJALADA KIDOGO UWANJANI

SADIO MANE ALICHANGANYA MAJALADA KIDOGO UWANJANI


SADIO Mane, winga wa Klabu ya Liverpool, jana alisahau kuanza kupiga goti moja chini ya uwanja kabla ya mchezo kuanza kati yao na Everton.

Baada ya Ligi Kuu England kurejeshwa kwani zilisimama kwa tangu Machi kutokana na janga la Virusi vya Corona kumekuwa na utaratibu kwa mechi zote zinazochezwa wachezaji wa timu zote mbili kupiga goti chini ikiwa ni ishara ya kupinga ubaguzi wa rangi duniani.

Hata jezi pia za wachezaji wote zimeandikwa, “Black Lives Matter,’. Baada ya refa kuruhusu wachezaji kupiga goti Mane alikosea kidogo na kuingia sehemu ya Everton, alipogundua amekosea alirejea kwa wachezaji wenzake na kupiga goti.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Goodison Park ulikamilika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu bila kufungana bao ndani ya dakika 90.

Liverpool ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 83 huku Everton ikiwa nafasi ya 12 na pointi zake 38 zote zimecheza mechi 30.

SOMA NA HII  AZAM FC: SIMBA WETU KABISA TUMEWACHAPA SANA, LEO TUTAPAMBANA