Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO…WASAUZI WAJIKUTA NJIA PANDA…YANGA WASHINDWE WENYEWE TU…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…WASAUZI WAJIKUTA NJIA PANDA…YANGA WASHINDWE WENYEWE TU…

Habari za Michezo

Marumo Gallants ipo kwenye mtego unaohitaji mbinu na akili nyingi sana kuutegua ili wafanikiwe.

Marumo ina mechi mbili (2) muhimu za maamuzi! Jumatano Mei 17, 2023 watacheza mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga ambapo tayari wako nyuma kwa mabao 2-0.

Siku tatu baadae, Jumamosi ya Mei 20, 2023 watakuwa mzigoni kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi ya Afrika Kusini dhidi ya Swallows.

Mechi zote zinaamua hatma ya Marumo Gallants, mechi dhidi ya Yanga itaamua timu ya kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mechi dhidi ya Swallows itaamua hatma ya Marumo kubaki kwenye Ligi au kushuka daraja.

Marumo Gallants ipo kwenye hatari ya kushuka daraja kutoka Ligi Kuu kwenda Ligi daraja la Kwanza. Ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 29 sawa na Chippa United na Maritzburg United.

Kwenye Ligi ya Afrika Kusini timu ya mwisho kwenye msimamo [Maritzburg United] inashuka moja kwa moja, timu ya pili kutoka mwisho [Chippa United] itacheza play-offs kujinusuru kushuka daraja.

Marumo Gallants, Chippa United na Maritzburg United zote zinalingana alama [29], kwenye msimamo wa Ligi zinatofautishwa na wastani wa magoli tu.

Maana yake Marumo ikipoteza mchezo wa mwisho wa Ligi dhidi ya Swallows halafu Chippa United na Maritzburg United zikishinda maana yake Marumo inashuka daraja moja kwa mojo.

SOMA NA HII  SAKATA LA KUTOLEWA KWA MKOPO....AKPAN AJIFANYA HAJUI KINACHOENDELEA SIMBA....AJITETEA NA KAMBI YA MISRI...