Home Habari za michezo KISA MKUDE…KIUNGO MNANIGERIA AVUTIKA KUJIUNGA SIMBA…AMMIMINIA SIFA ZA KIWANGO CHA LAMI….

KISA MKUDE…KIUNGO MNANIGERIA AVUTIKA KUJIUNGA SIMBA…AMMIMINIA SIFA ZA KIWANGO CHA LAMI….


KIUNGO wa kimataifa wa Nigeria, Victor Akpan anayetarajiwa kujiunga na klabu ya Simba msimu ujao amefunguka kitakachompeleka msimbazi huku akishindwa kuficha hisia zake kwa Jonas Mkude.

 Akpan aliyewahi kucheza Catsin ya Nigeria, JKU ya Zanzibar kisha kutimkia Majees ya nchini Oman kabla ya kujiunga na Coastal Union mwanzoni mwa msimu huu, siku chache zilizopita Mwanaspoti iliainisha kuwa mchezaji huyo tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili na anachongoja sasa ni msimu tu kuisha atue Msimbazi.

Akpan alisema kuwa Simba ni miongoni mwa timu zilizompelekea ofa ukiachana Black Leopard ya Afrika Kusini na klabu yake za zamani lakini kwake aliona kujiunga na Simba kunaweza kuwa ni maamuzi sahihi zaidi.

“Kutokana na uwezo wangu pamoja na kiwango nilichokionyesha msimu huu nafikiri umefika wakati wa mimi kwenda kucheza mashindano ya Kimataifa (CAF) na kati ya timu zilizoniletea ofa ni Simba ambayo msimu ujao itashiriki pia CAF,” aliendelea na kusema;

“Sio tu kushiriki CAF bali mimi kama mchezaji nahitaji zaidi kuwa sehemu nitakayoweza kuwa na mataji mbalimbali na pia naamini ndani yangu kuwa naweza kuipa timu mataji kama ambavyo nakaribia kuipa Coastal taji la kombe la shirikisho la Azam.

Aidha pia Kiungo huyo alisema katika maisha yake ya kucheza katika eneo la Kiungo hapa nchini kwake Jonas Mkude ndiye anayevutiwa nae zaidi.

“Natamani kucheza pamoja nae, ni kiungo mwenye ubunifu mguuni na anayejituma anapokuwa kiwanjani kitu ambacho kinamuongezea uimara na ubora ingawa pia uwezo wa Feisal Salum nautambua kwani nishawahi kucheza nae mazoezi kule Zanzibar na ninashangazwa kwanini hajawahi kufikiria kwenda kucheza nje ya nchi,” alisema Akpan.

Akpan alisajiliwa na Coastal Agosti mwaka jana na kupewa mkataba wa miaka miwili huku akiwa nguzo ya eneo la kiungo la timu hiyo ndani ya msimu huu.

SOMA NA HII  KISA 'UKATA'...AUSSEMS 'UCHEBE' AWAPIGA MKWARA MABOSI ZAKE KENYA...NI KAMA ALIVYOWACHANA SIMBA WAKATI ULE...