Home Habari za michezo KISA USAJILI WA AZIZ KI NA KAMBOLE…NABI ASHINDWA KUJIZUIA YANGA…ADAI KUNA MTU...

KISA USAJILI WA AZIZ KI NA KAMBOLE…NABI ASHINDWA KUJIZUIA YANGA…ADAI KUNA MTU ANAMTAFUTA…”SITAKI KUYUMBA”…


Yanga imemalizana na washambuliaji wawili hadi sasa lakini kama unadhani wamemaliza basi unakosea kwani kocha wao Nasreddine Nabi ametangaza kuwa mashine nyingine lazima ije tena kule mbele.

Yanga imemalizana na mshambuliaji Stephan Aziz KI ambaye hata kabla ya klabu hiyo haijathibitisha , staa mwingine ni Lazarous Kambole ambaye naye anakuja msimu ujao.

Nabi amesema kuwa amehakikishiwa na mabosi wa klabu hiyo kuwa atakuwa na KI na Kambole, lakini bado akatamka kwamba anataka mashine nyingine ya mabao.

Alisema anafikiria kuongeza mshambuliaji mwingine bora zaidi mbali na hao wawili ambaye atakuja kupambana na Fiston Mayele.

“Ndiyo nimeambiwa hao wachezaji wawili tutakuwa nao msimu ujao (KI na Kambole). Ni wachezaji bora sana, klabu kubwa kama hii ni fahari kuwa nao. Unajua najivunia kufanya kazi na wenye nguvu kama Injinia (Hersi Said) lakini nimemwambia bado nafikiria kuhitaji mtu mwingine zaidi,” alisema Nabi.

“Nitahitaji mshambuliaji mwingine, kuna aina ya mtu bora zaidi namtafuta sitaki kuyumba hata kidogo msimu ujao. Tunakwenda kwenye mashindano makubwa huko lazima uwe na watu wasio na mashaka angalau watatu, wapo ambao wataanza kwenye mechi na wengine kusubiri.

“Tutakapokuwa na timu bora ya mashindano ya CAF moja kwa moja tutakuwa na timu nzuri, huku ndani kitu kizuri zaidi ndoto zangu pia hazitofautiani na uongozi wa klabu hii, sote tunaitakia mafanikio makubwa msimu ujao.”

AMVUTIA KASI KAMBOLE

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wana wasiwasi na usajili wa Kambole wakidai hajacheza muda wa kutosha Kaizer Chiefs, lakini Nabi akacheka kisha akawataka watulie akisema ni jambo jema atakuja mapema na atampa dozi maalumu ikiwemo kumbadilisha nafasi. “Sioni tatizo sana. Kama wewe ni mshambuliaji mzuri ni mzuri tu, unaweza kuwa na mtu aliyecheza kwa ubora anakotoka kisha akaja hapa akapotea. Kambole namjua na nilikuwa namfuatilia,” alisema Nabi.

“Tayari tunaye Mayele ambaye yuko vizuri. Kama pia tukipata mtu mwingine ina maana aje mapema. (Kambole) tutakuwa na kazi naye kubwa ili arudi katika ubora wake akiwa hapa Yanga. Kitu kizuri ni mtu anayejua kufunga.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here