Home Habari za michezo KUELEKEA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU…FIFA WAPANGA KUTUMIA MAROBOTI BADALA YA WAAMUZI...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU…FIFA WAPANGA KUTUMIA MAROBOTI BADALA YA WAAMUZI WA KAWAIDA…


SHIRIKISHO la Soka Kimataifa (FIFA) lipo kwenye mkakati wa kutambulisha maroboti watakaokuwa waamuzi wa pembeni katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Qatar, Novemba mwaka huu.

Rais wa Shirikisho hilo Gianni Infantino imepania kutambulisha mfumo huo wa maroboti kuchezesha mechi za michuano hiyo badala ya marefa wa pembeni.

Majarabio ya mfumo huo yataanza kufanyika katika uwanja uliochezwa fainali ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu mwaka jana kabla ya kutambulishwa kwa mashabiki.

Mkutano wa viongozi wa wa FIFA kuhusu hiuo mfumo ulitakiwa kufanyika Qatar tangu Machi mwaka huu, hata hivyo ilipigwa kalenda baada ya vita kati ya Urusi na Ukraine kutibua mipango.

Kwa mujibu wa taarifa FIFA ipo tayari kuanzisha mfumo huo wa maroboti endapo viongozi wengine wataridhishwa kabla ya kuuzindua.

Endapo FIFA itapitisha mfumo huo itakuwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia kuchezwa na maroboti katika historia ya soka.

SOMA NA HII  KOCHA WA CHELSEA KUWAPA MAUJANJA CHAMA NA PHIRI....ISHU IKO HIVI..