Home Habari za michezo ILE ISHU YA SIMBA KUACHANA NA MASHINE ZA MAGOLI IKO HIVI…..HAIJAWAHI TOKEA…..

ILE ISHU YA SIMBA KUACHANA NA MASHINE ZA MAGOLI IKO HIVI…..HAIJAWAHI TOKEA…..

Habari za Simba leo

KLABU ya Simba imeonekana kuwashangaza wengi baada ya kuwaacha wachezaji wawili ambao walikuwa vinara wa mabao kwenye timu hiyo.

Simba juzi ilitangaza kuachana na mshambuliaji wao kinara wa mabao Jean Baleke ambaye kwenye ligi alikuwa na mabao manane, mawili nyuma ya kinara Stephen Aziz KI wa Yanga mwenye 10.

Pia timu hiyo imemuacha mchezaji Moses Phiri ambaye anashika nafasi ya pili kwenye ufungaji Simba akiwa amefunga mabao matatu kwenye ligi hadi sasa.

Hii inaonekana kuwa jambo la kushtua kwa kuwa kwa ujumla kwenye ligi Simba imefunga mabao 23, tu na wawili hao wamefunga nusu ya idadi hiyo lakini wameachwa.

Simba italazimika kuhakikisha kuwa washambuliaji wake wawili iliyowasajili Pa Omar Jobe na Fredrick Michael wanafanya kazi kubwa kwenye eneo la ufungaji, vinginevyo timu hiyo itakuwa na wakati mgumu wa kupata mabao kwenye ligi msimu huu kwa kuwa waliobaki akiwamo Johh Bocco na Kibu Denis, Esomba Onana na Saido Ntibazonkiza hawajaanza vyema katika utupiaji wa mabao msimu huu.

SOMA NA HII  YANGA YAWAFUATA KAGERA SUGAR KWA KUJIAMINI