Home Habari za Yanga HIZI HAPA KARATA ZA GAMONDI NA UBINGWA LIGI KUU…BACCA ASUGULISHWA BENCHI

HIZI HAPA KARATA ZA GAMONDI NA UBINGWA LIGI KUU…BACCA ASUGULISHWA BENCHI

BACCA AMKATAA MAMA YAKE...KUMBE ANALIPWA MAOKOTO YA KUMWAGA...BABA MZAZI AFUNGUKA

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema licha ya kuwapo kwa ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, wachezaji wake wamekuwa wakipambana uwanjani kusaka pointi kwa dakika zote kwa ajili ya kufikia malengo yao, jambo ambalo linampa
matumaini makubwa ya kutetea ubingwa wao, lakini hawajawa na uhakika kwa asilimia 100.

Yanga juzi waliendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kufikisha pointi 64 kileleni, bao hilo pekee likifungwa na Joseph Guede.

Gamondi alisema mechi ilikuwa ngumu sana licha ya kutokea mambo mengi ndani ya uwanja ikiwamo kutopewa penalti pamoja na kutengeneza nafasi nyingi kwa kushindwa kuzitumia, lakini wachezaji walipambana na kufanikiwa kupata bao hilo la ushindi.

“Tulicheza mpira mzuri, nimefurahi wachezaji walitulia na kufanikiwa kukusanya pointi kwa bao pekee la Guede, mchezaji mzuri na mshambuliaji wa mwisho amefanya kazi nzuri.

“Kuhusu Bacca (Ibrahim), si majeruhi bali nimefanya mabadiliko ya safu ya ulinzi kwa kumpumzisha kwa sababu ya kucheza mechi nyingi na mfululizo kulingana na jinsi ya ratiba ya ligi ilivyo kwa sasa,” alisema Gamondi.

Alieleza kuwa wako kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji la ubingwa, lakini bado hawajakuwa na asilimia 100 kwa hilo kwa sababu bado wana michezo mkononi na ligi haijaisha, hivyo wanatakiwa kuwa makini kusaka ushindi bila kuangalia waliopo chini yao wanafanya nini.
Kocha Mkuu wa Coasta Union, David Ouma, alisema wachezaji wake wamecheza vizuri licha ya Yanga kuwa na wachezaji wazoefu ambao waisaidia kufanikisha ushindi huo.

Alisema Yanga wamepata pointi tatu wakiwa pungufu baada ya mchezaji wake (Lawi) kupewa kadi nyekundu, hali ambayo wapinzani wao hao walitumia nafasi hiyo kupata bao moja.

β€œSio mchezo nzuri kwangu kwa sababu tumepoteza, ninaimani tungekuwa kamili wasingetufunga, kipindi cha kwanza tukiwa 11 kwa 11 hawakupatanafasi ya kufunga hadi dakika 69 tulienda 0-0 baada ya kadi nyukundu ndio wakatufunga,” alisema Ouma.

Aliongeza kuwa mechi ilikuwa ya ushindani mkubwa kwa timu zote mbili na anawapongeza wachezaji wake kufanya kile alichokielekeza kwenye uwanja wa mazoezi na kuhamisha uwanjani.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AINGILIA KATI ISHU YA DUBE NA AZAM..."ASHTAKIWE HUO NI UZEMBE