Home Habari za Yanga KUMBE YANGA WATUMIA MBINU HII KUFANYA USAJILI…RAIS AFUNGUKA KILA KITU A-Z

KUMBE YANGA WATUMIA MBINU HII KUFANYA USAJILI…RAIS AFUNGUKA KILA KITU A-Z

KUMBE YANGA WATUMIA MBINU HII KUFANYA USAJILI...RAIS AFUNGUKA KILA KITU A-Z

Rais wa Klabu ya Young Africans, Eng. Hersi Said amesema kuwa kila mchezaji mkubwa anataka kwenda kucheza kwenye klabu hiyo kutokana na malengo makubwa ya klabu, maono ya viongozi na mafanikio ambayo wamekuwa wakiyapata siku hadi siku.

Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na Bongo FM ikiwa timu yake iko mbioni kuubeba tena ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania kwa,ara ya tatu mfululizo.

“Ukweli ni kwamba kuna wachezaji kadhaa kutoka Klabu kubwa wanataka kujiunga na Klabu yetu. Ni kwa sababu wanaona uimara wa Uongozi, wadhamini na uwepo wa GSM.

“Pia mashabiki wetu ni sehemu ya usajili huwezi kuwakwepa mashabiki, wanaweza kukuonyesha mchezaji mzuri kwahiyo kuna wakati unapaswa kusikiliza sauti za mashabiki,” amesema Eng. Hersi.

SOMA NA HII  KISA KUFUNGA....'MZUNGU' WA SIMBA AFUNGUKA JINSI ALIVYOPAMBANA NA MASHABIKI INSTGRAM...'WALIKUWA WANASUMBUA'....