Home Habari za michezo BAADA YA KUONA SIMBA ‘KABANJULIWA’ JANA….YANGA KWENDA NA GIA HII KWA NAMUNGO…

BAADA YA KUONA SIMBA ‘KABANJULIWA’ JANA….YANGA KWENDA NA GIA HII KWA NAMUNGO…

Habari za Yanga leo

YANGA hawajasahau September 29, mwaka jana kitendo cha kuvuna alama dakika za mwisho dhidi ya Namungo FC mchezo wa mzunguko wa kwanza safari hii wanaingia kivingine katika duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi wa wapinzani hao.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Yanga ikiwa uwanja wa nyumbani walikutana na kibarua kigumu na kuvuna alama tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dakika za mwisho katika dimba la Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam.

Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kwa ndege kuelekea Nachingwea na hapo watapanda basi moja kwa moja kwenda Ruangwa Lindi na tayari kwa mchezo huo dhidi ya Namungo FC , leo uwanja wa Majaliwa.

Yanga wanahitaji ushindi katika mchezo huo kwa lengo la kuwaaacha mbali kwenye mbio za Ubingwa wapinzani wao Azam FC wakivuna pointi 43 sawa na Mabingwa hao watetezi wakiwa mbele kwa michezo mitatu na wakiwa nafasi ya tatu Simba kwa alama 36.

Kwenye michezo mitano timu hizo zimekutana tangu 2021 hadi 2023 wameshuka dimbani mara tano kwa kutoka sare mechi moja ikiwa Novemba 20, 2021 Namungo FC wakiwa nyumbani wakitoka sare ya bao 1-1.

April 22 na Desemba 17, 2022 Yanga walishinda mechi zote mbili nyumbani na ugenini, walivuna alama tatu kwa ushindi wa mabao 2_1 na mzunguko wa pili Namungo FC wakiwa nyumbani waliruhusu mabao 2-0.

Februari 4 , mwaka jana Yanga walifanikiwa kuvuna pointi zingine Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na September 20, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu Namungo FC waliwakazia Yanga na kuvuna alama tatu katika dakika za jioni.

Kuelekea mchezo wa kesho Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema maandalizi yameenda vizuri malengo makubwa na kuendelea na safari yao ya kukusanya pointi kila mechi kwa ajili ya kutetea ubingwa.

Amesema mechi itakuwa ya ushindani mkubwa kwa sababu mechi ya duru la kwanza Namungo FC, walionyesha mpira mzuri na kuwapa ushindani mkubwa na kufanikiwa kupata bao dakika za mwisho.

“Tumefanya maandalizi mazuri kukabiliana na Namungo FC, tunawafahamu mechi ya kwanza walitusumbua na sasa tunaingia kivingine kuhakikisha tunavuna pointi tatu ugenini,” amesema kocha huyo.

Alisema hutumia mechi za kuandaa siraha zake ya maangamizi ya robo fainalia ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alisema anafahamu ugumu wa michezo ya kimataifa na kutakiwa kufanya maandalizi kwa kusahihisha makosa yaliyofanyika kwenye michezo ya nyuma.

Ameeleza kuwa licha ya bado hawajajua wanakutana na nani lakini anaimani mechi za ligi zitamsaidia kuandaa kikosi chake vizuri kujiandaa na michezo ya robo fainali.

“Tunajiandaa na mechi za ligi ambazo tutazitumia kutafuta matokeo mazuri kuelekea kuvuna pointi tatu katika kila mechi hizi nne, lakini pia kutumia hizi mechi kujiandaa na robo fainali.

Mechi za makundi zilikuwa ngumu na ushindani mkubwa lakini vijana wamepambana kwa kila hatua na kufanikiwa kufika hatua ya robo kwa kuvuka malengo yetu,” alisema kocha wa Yanga,

Kikosi cha Yanga kimemaliza nafasi ya pili katika Kundi D wakiwa na pointi 8, kimerejea nchini jana kikitokea nchini Misri katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya Al Ahly inayongoza wakikusanya alama 12.

SOMA NA HII  KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA....VIGOGO WASUSIA NAFASI YA UENYEKITI....