Home Uncategorized DAVID KAMETA MAARUFU KAMA DUCHU ATUA SIMBA

DAVID KAMETA MAARUFU KAMA DUCHU ATUA SIMBA

 

 DAVID Kameta maarufu kama Duchu leo Agosti 15 ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Simba.

Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara akitokea Klabu ya Lipuli.

Kwa msimu wa 2019/20 akiwa Lipuli ambayo itashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao alitupia mabao matatu na kutoa jumla ya pasi saba.

Anaungana na Shomari Kapombe ambaye ni beki wa kulia ambaye naye ni mtambo wa kumwaga maji.

Msimu wa 2019/20 ametoa jumla ya pasi sita kati ya mabao 78 yaliyofungwa na Simba.

 

SOMA NA HII  MTANZANIA ASEPA NA TUNZO ULAYA BAADA YA KUTUPIA MABAO MANNE