Home Habari za michezo KISA UMRI MDOGO NA UWEZO WAKE….WINGA TELEZA AZUILIWA SIMBA…

KISA UMRI MDOGO NA UWEZO WAKE….WINGA TELEZA AZUILIWA SIMBA…


Kukiwa na tetesi za kutolewa kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao, winga chipukizi wa Simba, Jimmyson Mwanuke amepata mtetezi aliyeamua kumzuia Msimbazi kwa maelezo ni bonge la mchezaji ni vile tu hajapewa nafasi kubwa ya kukinukisha kikosini.

Nyota wa zamani wa Simba aliyewahi kukipiga timu nyingine kadhaa ikiwamo Pallsons, Mnenge Suluja alisema Mwanuke ni mchezaji mzuri, ila hajapata nafasi ya kutumika vyema hivyo kama ataskabizwa Msimbazi atailetea manufaa kama alivyokuwa akikiwasha Gwambina.

Mwanuke alijiunga na Simba msimu huu akitokea Gwmabina iliyoshuka daraja msimu uliopita kutoka Ligi Kuu kwenda Championship, lakini hajapata nafasi kubwa kikosi cha kwanza na pale anapoaminiwa amekuwa akitumika kama beki wa kulia na kuonyesha uwezo mkubwa.

“Binafsi naridhishwa na Jimyson Mwanuke na wachezaji wengine vijana wa Simba ni kijana mdogo na safari yake ni ya matumaini ameonyesha uwezo aaminiwe wala asitolewe kwa mkopo,” alisema Suluja na kuongeza

“Tulimuona mchezo dhidi ya Yanga alimudu vizuri na mechi hizi za mwisho wa msimu amecheza vyema anafaa kupewa nafasi kwa sababu ataletwa nani mzawa mwenye uwezo zaidi? Nafikiri wazawa waliopo wanatosha kwani wengi viwango vinafanana.”

Nyota wa zamani wa Kagera Sugar, George Kavila aliungana na Suluja akisisitiza wachezaji wazawa kupewa thamani na kutambua mchango wao pale wanapofanya vizuri na kuzibeba timu zao.

“Wazawa wengi wana mchango mkubwa kwenye timu zetu lakini nafikiri hatuwapi heshima inayostahili hasa wanahabari, tuwaheshimu wazawa wanapofanya vizuri na tuendelee kuwapa nafasi na sapoti,” alisema Kavila.

SOMA NA HII  HUYU HAPA STAA WA YANGA ANAYETAKIWA NA MARSEILLE YA UFARANSA...MWINYI ZAHERA TOA LA MOYONI KUHUSU DILI HILO..