Home Habari za michezo AHMED ALLY AINGILIA KATI ISHU YA DUBE NA AZAM…”ASHTAKIWE HUO NI UZEMBE

AHMED ALLY AINGILIA KATI ISHU YA DUBE NA AZAM…”ASHTAKIWE HUO NI UZEMBE

Habari za Simba leo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kitendo cha mshambuliaji wa Klabu ya Azam, Prince Dube kutokuwepo kwenye kikosi hicho ni uzembe wa timu hiyo.

Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Dube kutokuwepo ni udhaifu wa Azam FC, mchezaji wako ambaye una mkataba naye halafu akakosena kwenye timu ni mapungufu makubwa. Kitendo cha yule bwana kutokuwepo ni udhaifu wao Azam. Wewe mchezaji una mkatbaa naye anakaaje nje ya timu katikati ya msimu?

“Madai ya mchezaji ni kwamba ana mkataba unaoishia 2024 lakini huo wanaosema unaishia 2026, yeye hautambui. Lakini huu msimu haujaisha, kwa nini Dube hachezi? Huo ni udhaifu wako, mchezaji anapaswa kuutumikia mkataba wake.

“Azam walipaswa wawe na kesi nyingine ya kumshitaki mchezaji huyo kwamba hautumikii mkataba wake. Anatakatiwa autumikie mpaka mwisho wake,” amesema Ahmed,” amesema Ahmed Ally.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku

SOMA NA HII  AHMED ALLY AWACHONGEA YANGA TFF...USHINDI WAO UCHUNGUZWE...ATEMA CHECHE HIZI