Home Habari za michezo KUHUSU TZ KUFUNGWA 3-0 NA MOROCCO JANA….HUU HAPA UKWELI WA MAMBO USIOUJUA…

KUHUSU TZ KUFUNGWA 3-0 NA MOROCCO JANA….HUU HAPA UKWELI WA MAMBO USIOUJUA…

Habari za Michezo leo

LICHA ya timu ya taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ kuanza vibaya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa kupoteza dhidi ya Morocco kwa mabao 3-0, bado ina nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo huko Ivory Coast.

Taifa Stars iliuanza mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro ikiwa na mpango wa kujilinda zaidi kufuatia kikosi chake kuundwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye sifa ya kuzuia huku jukumu la kushambulia likiwa kwa Mbwana Samatta, Charles M’Mombwa na Tarryn Allarakhia.

Licha ya Stars kuingia na mpango wa kuzuia huku ikionekana kushambulia kwa kushtukiza ilijikuta ikiruhusu bao la kwanza katika dakika ya 30 baada ya Aishi Manula kutema faulo ya Hakim Ziyech kisha, Romain Saiss akamalizia.

Morocco ilionekana kuwa na umiliki mkubwa wa mchezo kiasi cha kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche kufanya mabadiliko kwa kumtoa Tarryn ambaye alichemka na nafasi yake akaingia Simon Msuva aliyewajibika kushambulia kutokea pembeni.

Stars ilijikuta katika mazingira magumu zaidi katika kipindi cha pili hasa baada ya kuwa pungufu kutoana na Novatus Dismas kuonyeshwa kadi ya pili ya njano iliyofuatiwa na nyekundu katika dakika 70.

Dakika saba baadaye Morocco ilijipatia bao la pili kupitia kwa Azzedine Ounahi kisha kufunga la tatu katika dakika ya 80 kupitia kwa Youssef En-Nesyri.

Licha ya Stars kufanya mabadiliko kadhaa ikiwemo kuingia kwa Morice Abraham, Feisal Salum huku wakitoka Mudathiri Yahya na Samatta bado haikuwa suluhu ya kunusurika na kipigo hicho. Pamoja na matokeo hayo, beki wa kati wa Stars, Bacca ni miongoni mwa wachezaji wa Stars ambao walionekana kuonyesha kiwango kizuri, nidhamu yake kwenye kulinda ilikuwa kubwa huku akionekana mtulivu.

Taifa Stars inatakiwa kusahau matokeo ya mchezo huu wa leo na badala yake kuelekeza nguvu kwenye michezo yake miwili iliyosalia kwenye hatua hiyo ya makundi ambayo ni dhidi ya Zambia, Januari 21 na DR Congo, Januari 24 ili kuweka historia ya kuvuka hatua ya makundi.

SOMA NA HII  TAIFA STARS 'HOI BIN TAABANI' VIWANGO VYA FIFA..YAZIDI KUPOROMOKA KWA KASI YA KIMBUNGA...