Home Habari za michezo KUFUZU AFCON 2023…’HOMA YA JIJI’ AIPA DAWA TAIFA STARS…AANIKA SIRI ZA...

KUFUZU AFCON 2023…’HOMA YA JIJI’ AIPA DAWA TAIFA STARS…AANIKA SIRI ZA KUICHAKAZA UGANDA MAPEMAAA…


ACHANA na matokeo ya jana usiku dhidi ya Algeria, Taifa Stars imeumwa sikio na malegendari wa zamani, ikitakiwa kujiimarisha eneo la ushambuliaji na mabeki kabla ya kuivaa Uganda katika mechi zao zijazo za Kundi F za kufuzu fainali za Afcon 2023.

Stars itakutana na Uganda, Septemba mwaka huu katika mechi mbili ambazo zitaiweka pazuri au mbaya ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika Ivory Coast kabla ya Machi mwakani kukamilisha mechi za mwisho dhidi ya Niger na Algeria.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Iddi Moshi ‘Mnyamwezi’ alisema; “Uganda ina timu nzuri na wako fiti. Niliwaona mechi na Algeria, inacheza kwa ushirikiano hivyo sisi tunapaswa kuikabili kwa tahadhari lakini muhimu ni kutumia nafasi nzuri za kufunga tunazopata.”

“Stars inahitaji utulivu tu kwenye safu ya ulinzi, ila umakini kwa washambuliaji, lakini sehemu nyingine kote tuko vizuri.” Naye mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Stars, Makumbi Juma’ Homa ya Jiji’ alisema timu hiyo inahitaji kujiandaa kikamilifu kuikabili Uganda ili kupata ushindi katika mechi zote mbili.

“Uganda inacheza kitimu, wachezaji wake hawakati tamaa, hivyo Stars inahitaji jambo moja tu kuwa watulivu hasa kwa wachezaji wanaocheza mbele kwani ukiangalia nafasi za kufunga wanapata lakini wanashindwa kuwa na autulivu katika kumalizia,” alisema Makumbi, huku kiungo wa zamani wa Tukuyu Stars, Yanga na Taifa Stars, Sekilojo Chambua alisema Stars inatakiwa kujiandaa vizuri kwani ina kibarua kizito katika mechi ijazo kwani Uganda ni hatari.

“Wengi wanaweza kuiona Uganda ni timu ya kawaida kwa vile ni majirani zetu, ila ni moja ya timu iliyo fiti na hatari inapokuwa nyumbani hivyo ni lazima Stars ijiandae vizuri,” alisema Chambua, huku Zamoyoni Mogella alisema; “Nidhamu ya mchezo na kumuheshimu mpinzani basi matokeo unapata.”

SOMA NA HII  HIZI HAPA SALAMU ZA SIMBA KWA YANGA....ZATINGA AVIC TOWN KIBABE....