Home Habari za michezo VIGOGO SIMBA WADINDISHIANA KUHUSU NANI WA KUACHWA KATI YA MUGALU NA BOCCO…KAGERE...

VIGOGO SIMBA WADINDISHIANA KUHUSU NANI WA KUACHWA KATI YA MUGALU NA BOCCO…KAGERE HANA MTETEZI…


Mastraika John Bocco na Chris Mugalu waliong’ara msimu uliopita wakiwa vinara wa mabao wa Simba na Ligi Kuu Bara msimu uliopita, wamewagawa mabosi wa klabu hiyo ya Msimbazi juu ya nani anayetakiwa kutemwa kwa ajili ya kikosi kipya cha msimu ujao.

Bocco aliye nahodha wa Simba, ndiye aliyekuwa Mfungaji Bora wa msimu uliopita akifunga 16, akifuatiwa na Mugalu aliyemaliza wa pili akitupia mpira nyavuni mara 15, lakini kwa msimu huu wameyumba na kuifanya timu kupoteza makali iliyokuwa nao awali.

Sio Bocco na Mugalu tu, lakini hata washambuliaji wengine wa timu hiyo akiwamo, Meddie Kagere na Kibu Denis nao wamewagawa viongozi wa Simba juu ya maamuzi kama watemwe wote au baadhi yao waachwe kupisha majembe mapya kikosini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba mabosi wa Simba wanachekecha vichwa juu ya washambuliaji walionao sasa, wengi wao wakitaka wapigwe chini na kubakishwa mmoja tu atakayeongezewa nguvu na majembe mapya yanayotarajiwa kusajiliwa.

Taarifa ni kwamba Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, tayari mezani mwao wana majina ya wachezaji wanaotakiwa kupigwa chini wakiwamo wa nafasi ya ushambuliaji, lakini kuna mgawanyiko wa nani abakishwe.

Chanzo hicho kilisema, washambuliaji wote walikuwa wazuri na msaada mkubwa na kila mmoja anao mchango wake ndani ya timu hiyo kitu kinachowachanganya kutokana na msimu huu kuonekana kupwaya klidogo. Kagere amefunga mabao saba sawa na Kibu aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbeya City, huku Bocco akiwa na matatu baada ya kukaa muda mrefu bila kutupia katika Ligi Kuu, ilihali Mugalu akiwa hana bao lolote hadi sasa licha ya kupata nafasi ya kucheza.

“Linapokuja jambo la kuboresha timu kwa kupunguza na kuongeza wachezaji hakuna mchezaji ambaye yuko juu ya timu na hicho sio kituo cha kulelea watu inatakiwa kutoka na kuingia wengine ili timu iweze kufikia malengo,” alisema mtoa habari huyo.

Mtoa habari huyo alisema, hata wao wanashindwa kuelewa shida ya wachezaji hao msimu huu, akimtolea mfano Bocco ambaye anaumwa leo anapona kesho na kushindwa kuonyesha mchango wake.

SOMA NA HII  MSAUZI KUPEWA U-CEO SIMBA....KAJULA AANZA KUAGA WACHEZAJI....ISHU NZIMA IKO HIVI...

“Kazi ipo kweli kweli kuna wanaosema Mugalu abakie wengine atoke, Kagere atoke(huyu hakuna anayetetea abaki), Bocco atoke mara wengine abakie mvutano unakuwa hapo, sisi Simba wachezaji wanaoachwa wanajijua japokuwa bado hatujawaambia tunasubiri mechi ziishe,” kilisema chanzo hicho.

Kuhusu Kibu naye anapewa nafasi na kuungwa mkono kusalia ndani ya msimu ujao na hata katika ripoti ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pablo Franco alimpendekeza kubaki.