Home Habari za michezo MASHABIKI YANGA WAISIMAMISHA DAR….KISHONDO CHAKE SIMBA WAKASOME AISEE…GSM AWA HABARI YA MJINI…

MASHABIKI YANGA WAISIMAMISHA DAR….KISHONDO CHAKE SIMBA WAKASOME AISEE…GSM AWA HABARI YA MJINI…


Nyomi ya mashabiki waliojitokeza kuipokea Yanga ambayo inasindikizwa na eskoti ya Polisi imefunga njia na kusababisha foleni kubwa barabara zote.

Yanga tayari wameshatoka uwanja wa ndege wanaelekea Jangwani wakipita mtaa wa Msimbazi na shughuli hiyo imesababisha foleni upande wa barabara inayoenda Gongo la Mboto na mjini.

Mashabiki wa timu hiyo wanaongozana na msafara wa timu huku wakiimba bila kuchoka GSM na kutaja jina la Fiston Mayele na kushangilia staili yake ya kutetema.

Polisi wanaongoza msafara pia hawapo nyuma kwa kukimbizana na msafara kuhamasisha mashabiki waondoke barabarani ili msafara uwahi kufika eneo la tukio.

SOMA NA HII  HATMA YA BOCCO SIMBA SHAKANI...MASTAA WENGINE WANAOWEZA KUKATWA HAWA HAPA....