Home Habari za michezo MOSES PHIRI AENDELEA KUZICHEZESHA REDE SIMBA NA YANGA….AFUNGUKA MUSTAKABALI WAKE NA ZANACO…

MOSES PHIRI AENDELEA KUZICHEZESHA REDE SIMBA NA YANGA….AFUNGUKA MUSTAKABALI WAKE NA ZANACO…


MSHAMBULIAJI wa Zanaco, Moses Phiri amekiri mkataba wake na timu yake hiyo unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Phiri alisema mkataba wake na waajiri wake unamalizika mwishoni mwa mwezi huu huku akiweka wazi kuwa bado ajajua ni wapi anaenda ataweka wazi baada ya mambo yake kukamilika.

“Ni mchezaji wa Zanaco hadi mwisho wa mwezi huu na kuhusu mazungumzo na timu nyingine yoyote ni siri yangu na timu hiyo lakini mambo yakiwa sawa nitaweka wazi ni wapi nitacheza,” anasema.

Phiri alijiunga na Zanaco akitoka Buildcon ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili katika msimu wake huu wa mwisho amefunga mabao 14.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29  ndani ya misimu yote amefunga mabao 31 kwenye mashindano ya kimataifa akiwa amecheza mechi nane amefunga mabao matatu na kutoa pasi iliyozaa bao moja.

Staa huyo wa Zanaco imethibitika kuwa tayari amemalizana na Simba kwaajili ya kuitumikia kwenye msimu mpya wa 2022/23 na atatua nchini wakati wowote kuanzia sasa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAARABU...MASTAA WOTE YANGA KUPIGWA CHINI....GAMONDI AFUNGUKA HILI..