Home Habari za michezo KAMA ULIKUWA HUJUI…YANGA WAKIBEBA KOMBE LA LIGI KUU TU…WANALAMBA BILIONI 4 ‘CASH’…MCHANGANUO...

KAMA ULIKUWA HUJUI…YANGA WAKIBEBA KOMBE LA LIGI KUU TU…WANALAMBA BILIONI 4 ‘CASH’…MCHANGANUO HUU HAPA…


KIASI kikubwa cha fedha ambacho Yanga itakivuna mwishoni mwa msimu kinaipa jeuri ya kunasa mastaa wasiopungua watatu kutoka katika timu yoyote barani Afrika na ikamudu kuwalipa mishahara na posho bila presha kwa mkataba wa miaka miwili.

Ikiwa itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Yanga itajihakikishia kitita kisichopungua Sh 4 bilioni ambacho kinatokana na mikataba minono ambayo imesaini na kampuni tofauti lakini fedha za zawadi kwa washindi wa Ligi. Kiasi kikubwa cha fedha itavuna kupitia mkataba wake wa maudhui na kampuni ya Azam Media ambao kuna kipengele kinachoipa fursa ya kupata kitita cha Sh 3 bilioni kama bonasi kwa kutwaa ubingwa au kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi kila msimu.

Timu hiyo itapata pia kiasi cha Sh 500 milioni kutoka Azam Media kama fedha za bonasi au zawadi kwa bingwa wa Ligi Kuu ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba wa haki za matangazo ya ligi baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga pia inaripotiwa itapata bonasi ya Sh 500 milioni kutoka kwa wadhamini wao wengine, kampuni ya GSM ikiwa watatwaa ubingwa wa ligi pia watapewa kiasi cha Sh 100 milioni na mdhamini wao mkuu, kampuni ya Sportpesa.

Jina la nyota linalotajwa na vigogo wa Yanga ni mshambuliaji wa Burkina Faso anayeichezea Asec Mimosas, Aziz Ki ambaye kwa mujibu wa ripoti, tayari ameshafikia makubaliano ya awali.

Iko hivi, Aziz inadaiwa atalipwa mshahara wa Dola 5,000 (Sh 11 milioni) kwa mwezi ambapo kwa kipindi cha miaka miwili, Yanga itamlipa mshahara wa jumla kiasi cha Dola 120,000 (Sh 279 milioni).

Ikisajili mastaa watano na kuwalipa kiasi hicho cha fedha kama mshahara, maana yake Yanga itatumia kiasi cha Dola 600,000 (Sh 1.3 bilioni) kwa mwaka kuwalipa mshahara na kwa miaka miwili, Yanga itatumia kiasi cha Sh 2.6 bilioni kuwalipa nyota hao.

Katika fungu la Sh 4 bilioni ambazo itapata, Yanga itabakia na kiasi cha Sh 1.4 bilioni (Dola 600000) ambacho kinaweza kutumika kama ada ya usajili ya wachezaji hao kwa kila mmoja kupata wastani wa Dola 150,000 (Sh 349 milioni).

SOMA NA HII  KISA MAYELE...BARNABAS AIBUKA NA HILI...AGUSIA ISHU YA WAZAWA...

Kwa mujibu wa mtandao wa transfermarkt unaojishughulisha kufanya tathmini ya bei za wachezaji na thamani zao, kuna nyota zaidi ya 10 katika klabu mbalimbali barani Afrika ambao thamani zao sokoni kwa sasa ni Dola 150,000 au chini ya hapo hivyo Yanga inaweza kuwapata wakicheza kwa nafasi tofauti.

Baadhi ya wachezaji hao ni mabeki, Nathan Idumba (Cape Town City), Chadrack Isaka Boka (FC Lupopo), Sidi Yacoub na Jacques Themopeie (AS Vita), Moses Phiri (Zanaco), John Ching’andu (Zesco United), Prince Dube (Azam), Wonlo Coulibaly na Ibrahim Bance (Asec Mimosas) pamoja na Richard Boro (FC San Pedro).

Mjumbe wa Kamati ya Usajili na Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said alilithibitishia Mwanaspoti kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanasajili nyota ambao wataifanya izidi kuwa tishio msimu ujao.

“Kikosi chetu kimeonyesha mafanikio makubwa msimu huu lakini tuna mashindano ya kimataifa msimu ujao ambayo mkakati wetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri hivyo tutahakikisha tunasajili wachezaji wenye viwango bora zaidi ambao watatuwezesha kutimiza malengo hayo,” alisema Hersi.

Kwa upande wa, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kwa kushirikiana na wadhamini wao kampuni ya GSM, watafanya usajili utakaotikisa sio tu hapa nchini bali Afrika kwa ujumla. Kocha Nabi Mohammed amesema watasajili kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia ubora.