Home Uncategorized SIMBA WAPIGA MATIZI YA MWISHO LEO, VITA YAO KESHO INA VIGINGI VIKALI...

SIMBA WAPIGA MATIZI YA MWISHO LEO, VITA YAO KESHO INA VIGINGI VIKALI MBELE YA MBEYA CITY


KIKOSI cha Simba leo kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho, Juni 24 dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, majira ya saa 10:00.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck inaipigia hesabu Mbeya City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Amri Said ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Simba akiwa ni beki.

Mazingira ya baridi yameonekana kuwa changamoto kwao ambapo wachezaji wameonekana wakiwa wakifanya mazoezi wakiwa na mizura kichwani pamoja na sweta.

Kazi kubwa itakuwa ni kusaka pointi tatu kwa kila timu ambapo kila kocha ana hesabu zake kulingana na mazingira ya kile anachohitaji.

Sven amesema kuwa anahitaji pointi tatu ili kusogelea nafasi ya kutwaa ubingwa huku Said akiwa na hesabu za kusepa na pointi tatu ili kujinusuru kutoka hatari ya kushuka daraja.

Mbeya City ikiwa imecheza mechi 30 kibindoni imejikusanyia pointi 30 huku Simba ikiwa imekusanya pointi 75 baada ya kucheza mechi 30.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar, Simba ilishinda mabao 4-0 mbele ya Mbeya City. Hivyo utakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani.

SOMA NA HII  KAMATI INAYOSHUGHULIKIA SAKATA LA MORRISON YAAHIDI KUTENDA HAKI