Home Uncategorized DILUNGA – MASHARTI YA MPENZI WANGU YAMENISAIDIA ..!!

DILUNGA – MASHARTI YA MPENZI WANGU YAMENISAIDIA ..!!

STAA wa Simba, Hassan Dilunga ‘HD’ amedai kwamba mpenzi wake pamoja na kocha wa sasa, Sven Vandenbroeck wamekuwa busta ya yeye kutamba Msimbazi.

Dilunga chini ya Patrick Aussems hakuwahi kupachika mabao kama ilivyo kwa Sven alikotupia manane sasa.

Dilunga alisema chini ya Sven amekuwa akimtumia zaidi kwenye eneo la kushambulia kuliko nyuma alikokuwa akimpanga Aussems.

Kuhusu mpenzi wake anasema; “Nilikaa na mpenzi wangu (amemficha jina)kabla ya msimu huu kuanza tulikubaliana kuwa anataka kuniona namaliza msimu nikiwa na mabao saba katika ligi jambo ambalo nililikubali na kumuahidi nitafunga mabao hayo na yatakuwa kama zawadi kwake.

“Nashuruku Mungu kabla ya msimu kumalizika nimelitimiza hilo baada ya kufunga katika mechi ya Mwadui juzi,” alisema.

“Kubwa ambalo nimefanikiwa katika malengo yangu ni kufuata maagizo ambayo napewa na Sven, ndio maana chini yake nimefunga mabao mengi zaidi na bado naendelea,” alisema Dilunga ambaye Simba imemuongezea mkataba wa miaka miwili.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII