Home Habari za michezo RASMI….INJINIA HERSI SAID RAIS MPYA YANGA….DK MSOLA AOGOPA AIBU YA KUSHINDWA UCHAGUZI…ASUSA...

RASMI….INJINIA HERSI SAID RAIS MPYA YANGA….DK MSOLA AOGOPA AIBU YA KUSHINDWA UCHAGUZI…ASUSA KURUDISHA FOMU….


Wakati Kamati ya uchaguzi ikitoa orodha ya wagombea waliopitishwa, Dk Mshindo Msolla jina lake halimo katika wagombea hao huku Injinia Hersi Said akiachiwa kuwa mgombea mwenyewe.

Orodha ambayo imetolewa na kamati hiyo imempitisha Hersi kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga Malangwe Mchungahela amesema wakati wakipitia fomu hizo hawakuiona ya Msola ambaye ni Mwenyekiti anayeondoka.

“Hatujaziona fomu za Dk Msolla, inawezekana hajarudisha kwetu baada ya kuzichukua, tulikuwa tunapitia fomu ambazo zimerudishwa kwenye kamati kwa wagombea ambao walichukua,” amesema Mchungahela.

Ingawa Dk Msolla hakupatikana taarifa zinadai Mwenyekiti huyo ameamua kuachana na mpango wa kugombea tena baada ya kumaliza muda wake.

Katika wagombea wa nafasi ya makamu wa rais Arafat Haji na Suma Mwaitenda wamepitishwa kugombea nafasi hiyo.

SOMA NA HII  KWA SURA MPYA YANGA , KUNA JAMBO LINAKUJA