Home Habari za michezo DEAL DONE….AZIZ KI AMALIZANA NA YANGA ….ASAINI MIAKA MIWILI ILIYOSHIBA KUKIPIGA JANGWANI…INJINIA...

DEAL DONE….AZIZ KI AMALIZANA NA YANGA ….ASAINI MIAKA MIWILI ILIYOSHIBA KUKIPIGA JANGWANI…INJINIA HERSI KAFANYA YAKE…


IMEISHA hiyooo. Habari ziwafikie wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa sasa ni uhakika msimu ujao eneo la ushambuliaji la timu hiyo atakuwapo staa kutoka Burkina Faso, Stephane Aziz Ki baada ya kumalizana na klabu hiyo na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Kama mtakumbuka juzi  Aziz Ki alifichua juu ya kujiandaa kukutana uso na uso na Injinia Hersi Said ili kukamilisha dili lake lililokuwa limefikia kati ya asilimia 80-90 na jana mchana mambo yalikamilika na sasa Yanga ina uhakika naye.

Hatua ya KI kusaini Yanga ni hitimisho la ushindi kwa klabu hiyo kupitia uwezeshaji wa wafadhili wao GSM walioanza kupambana na saini ya mshambuliaji huyo, ikichuana na klabu kadhaa ikiwamo Simba iliyokuwa inampigia hesabu tangu ilipomuona katika mechi zao za Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, akiwa na Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Jana nchini Ivory Coast, usajili huo ulikamilishwa na kwamba ulikamilika chini ya Hersi aliyemfuta baada ya awali kuanzisha mchakato ulioanzia jijini Berkane, Morocco.

Ingawa jana KI hakupokea , lakini mabosi wa Yanga walilithibitishia kwamba, fundi huyo anayejua kufunga vizuri mabao ya mguu wa kushoto ameshasaini mkataba wa miaka miwili.

“Tumeshamalizana naye kwa sasa ni mchezaji wetu kwa msimu ujao. Haikuwa kazi rahisi kwa mara nyingine tena GSM wamefanikisha usajili mkubwa kwa msimu ujao,” alisema bosi huyo ambaye yumo ndani ya sekretarieti ya klabu hiyo inayonukia kuchukua makombe yote makubwa yanayofanyika Tanzania Bara.

Mapema siku tatu zilizopita KI alisema kwamba usajili wake kutua Yanga ulibakiza kama asilimia 10 tu huku akidai kuwa kuna bosi wa vinara hao wa ligi ya bara kusafiri kwenda kumalizia mchakato huo.

“Kila kitu kinakwenda vizuri, kuna uwezekano mkubwa nikaja kucheza Tanzania. Kuna mtu nitakutana naye wiki ijayo kama ikiwa hivyo kila kitu kitamalizika,” alisema KI akiliambia Mwanaspoti.

Kufanikiwa kwa Yanga kumnasa KI kunaifanya kushinda vita na klabu kubwa za Kaskazini zikiwemo RS Berkane ya Morocco, Zamalek ya Misri na JS Saoura ya Algeria zilizokuwa zikiiwania saini ya mshambuliaji huyo alioyeitungua Simba mabao mawili katika mechi za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwan na Asec.

SOMA NA HII  NUSU MSIMU TU...TAYARI MAYELE KASHAVUNJA REKODI YAKE NA ANAELEKEA KUWEKA HII MPYA...