Home Habari za michezo KISA MECHI YA VIPERS NA SIMBA…KIBU DENIS KUWA NNJE KWA WIKI MOJA…ISHU...

KISA MECHI YA VIPERS NA SIMBA…KIBU DENIS KUWA NNJE KWA WIKI MOJA…ISHU NZIMA IKO HIVI….

Habari za Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis atakuwa nje ya uwanja kwa takriban wiki moja kutokana na majeraha aliyoyapoata katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

Daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo amesema Kibu amepata maumivu ya mguu na baada ya vipimo anahitajika kuwa nje kwa muda wa wiki moja ili kupona kabisa.

“Kibu amepata maumivu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Vipers, haikuwa mbaya sana lakini inabidi akae nje ya uwanja kwa wiki moja kabla ya kuanza mazoezi,” alisema Dk Edwin.

Simba inatarajia kushuka dimbani kesho kwenye mchezo wa Uhuru katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 16 Bora dhidi ya African Sports na kisha, Marchi 7, 2023 watawakaribisha Vipers kutoka Uganda kwenye Ligi ya Mabibigwa Afrika.

SOMA NA HII  NI YANGA TENA....WABEBA TAJI LA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA MBINDEEE...COASTAL UNIONI WAKIFA KIUME...