Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUACHWA..MORRISON AIGOMEA SIMBA…MAPYA ZAIDI YAFICHUKA ISHU YA KUFUKUZWA

SIKU CHACHE BAADA YA KUACHWA..MORRISON AIGOMEA SIMBA…MAPYA ZAIDI YAFICHUKA ISHU YA KUFUKUZWA


BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Simba amegomea kurudi ndani ya timu hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa kutokuwa na maelewano mazuri na moja ya viongozi wenye maamuzi makubwa.

Nyota huyo ambaye alisimamishwa kwa muda na mabosi wa Simba kwa kile ambacho kilieleza kwamba anashughulikia matatizo ya kifamilia mkataba wake unameguka mwisho wa msimu huu.

Na muda ambao alipewa mapumziko kwa makubaliano ya pande zote mbili ni mpaka mwisho wa msimu utakapoisha.

Mtu wa karibu wa Morrison amesema kuwa hakukuwa na matatizo yoyote ya kifamilia ambayo alikuwa anashughulikia isipokuwa kuna mtu alikuwa hakubali uwepo wake ndani ya timu hiyo.

“Kuna kiongozi ndani ya Simba alikuwa hapendi uwepo wa Morrison hasa kwa kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi ambazo zilikuwa zinaihusu Yanga jambo ambalo lilikuwa linawaumiza.

“Hana tatizo lolote na hata taarifa ambayo amepewa ilimshangaza hivyo aliamua kuondoka ndani ya Simba na hataongeza mkataba mwingine licha ya benchi la ufundi kuhitaji huduma yake,” ilieleza taarifa hiyo.

Morrison aliweka wazi Mei 13,2022 ni wakati mgumu kwake kutokuwa kwenye kikosi cha Simba kutokana na masuala ya kifamilia na alikuwa anaamini kwamba atarejea tena kutimiza majukumu yake.

Kwa sasa Morrison yupo Ghana akishughulika masuala yake binafsi na inaelezwa kuwa atarejea kwa mara nyingine kucheza ndani ya ardhi ya Tanzania lakini sio Simba.

Mabosi wake wa zamani Yanga wanapewa nafasi ya kupata saini yake.

SOMA NA HII  KISA KADI NYEKUNDU KWA TIMU PINZANI...HITIMANA AFICHUA MCHEZO NYUMA YA PAZIA...