Habari za michezo

MORISSON AZIDI KUIANIKA SIMBA….AFUNGUKA A-Z TUHUMA ZA KUCHUKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE KAMBINI…

admin July 1, 2022 3:46 am


Baada ya Sintofahamu ya muda mrefu juu ya hatma ya Mchezaji Bernard Morisson ndani ya Klabu ya Simba SC, huku wengine wakimuhusisha na Kujiunga na watani wao wa Jadi Yanga.

Hatimaye Morisson amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya kinachoendelea baina yake na waajiri wake ambao ni Simba SC.

Kwa sasa Morisson amerejea Jijini Dar es Salaam, na anajiandaa kuanza maisha mapya katika Klabiu ya Yanga lakini miongoni mwa machache aliyozungumza Morisson ni kuwa;

“Mkurugenzi aliniita ofisini kwake, nikaenda na ndipo aliponiambia kwamba wachezaji wenzangu wamekasirika na hawataki niendelee kuja mazoezini na makocha nao wanalalamika kwamba siwaheshimu, kwa hiyo malalamiko yamekuwa ni mengi kukuhusu mimi”

“Lakini nilisema hapana, mbona wachezaji hao hao ndiyo wanaonipigia simu mara kwa mara nisipoonekana mazoezini wakiniuliza naendeleaje? Jeraha langu linaendeleaje?” Anasema Morrison.

UNAAMBIWA BAADA YA BWALYA NA WAWA…ANAYEFUATA KUAGWA SIMBA NI KAGERE..SABABU KUBWA NI HII HAPA…. KUELEKEA MSIMU UJAO WA MASHINDANO YA CAF…KIGOGO AJIAPIZA YANGA KUIFUNIKA REKODI YA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply