Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa simbana raia wa ghana, benard efua morrison amemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, samia suluhu hassan kumpatia kibali cha kumuwezasha kuishi nchini tanzania (passposrt) kama raia wa tanzania kwa kuwa anaipenda sana tanzania.
Morrison amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online na kuongeza kuwa, hata kama hataweza kucheza klabu yoyote nchini Tanzania, lakini ana shauku ya kuendelea kubaki Tanzania katika maisha yake yote kama Raia wa Tanzania kutokana na ukarimu wa wananchi wake.
“Nimekuwa nikizungumza na Mwana FA (Mbunge wa Muheza) anifanyie mpango nipate passport ili niishi hapa hapa Tanzania kama Raia halali, lakini naona yuko bize kila siku ananiambia subiri kesho, subiri kesho, hata Fredy Vunjabei nimeshamwambia.
“Ninakuuomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu unipatie passport ili niweze kuishi Tanzania kama raia, kama nyumbani, ninaipenda Tanzania. Watanzania wananipenda sana kuliko hata nyumbani Ghana wanavyonipenda, hata Timu ya Taifa (Taifa Stars) nitacheza.
“Wakati nikiwa Yanga, mashabiki wa Simba walikuwa wananiponda kwenye mitandao ya Kijamii, lakini ukikutana nao mnacheka wanakupa pesa, vilevile nilivyokwenda Simba, mashabiki wa Yanga wanakuponda mtandaoni lakini ukikutana nao wanakupa pesa, ninawapenda sana Watanzania, natamanani sana niendelee kuishi Tanzania miaka yangu yote,” amesema Morrison.